Monday, June 10, 2013
Suala la Serikali tatu Tanzania.
Mbeya/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo yatakoma.”
Msimamo wa Sumaye
Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.
Sumaye anaungana na wanasiasa wengine waliopinga muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wengine wakiwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM) Profesa Juma Kapuya, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba na Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Daftari.
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiwa Johannesburg, Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, alisema Serikali tatu zinaweza kutikisa Muungano.
“Huwezi kutatua matatizo kwa Serikali tatu... unaweza kuyaongeza kwani kutakuwa na Serikali tatu na marais watatu... kama kuna mvutano baina ya Serikali mbili ukiongeza ya tatu inaweza kuwa na mvutano zaidi,” alisema na kuongeza:
Lipumba: Katiba ya Bara kwanza
Profesa Lipumba alisema hakuna mantiki ya kupiga kura ya maoni ya Katiba ya Muungano bila kuwa na Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mapendekezo ya msingi ya CUF ni kwamba, kura ya maoni isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Alisema licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya kazi nzuri ya kuratibu maoni bila kushinikizwa na matakwa ya CCM, kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo yameachwa kwenye rasimu.
“Huwezi kuacha vitu kama umilikaji wa ardhi, maliasili na rasilimali za nchi, elimu, afya na mazingira ya kukuza uchumi na uhuru wa Serikali za mitaa. Rasimu imeshughulikia mambo ya Muungano.”
“Maoni ambayo CUF tuliyatoa ikiwamo muundo wa Serikali tatu, kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, Rais kutangazwa baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, Spika kutokuwa mbunge na mengineyo yamepata nafasi.”
Imeandikwa na Brandy Nelson, Ibrahim Yamola na Aidan Mhando
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment