Thursday, June 27, 2013

Tamta Day (2)

 Wakaazi wa Tanga wakiwalaki wanafunzi wa Shamsiya waliokuwa wakitoka kuzuru makaburi ya Masheikh.

 Muddir Kigoda akiwa amestarehe ndani ya gari kurudi makao makuu ya Shamsiya (Tamta).

 Watu wa rika lote hutambua kuwa msimu huu ni msimu wa Tamta Day, hivyo hujipanga barabarani kuwalaki wanafunzi wa Sheikh Muhammad Bin Ayoub.

 Magari yalikuwa mengi kiasi ilibidi utumike utaratibu mzuri wa kuyapanga.
 Misafara ya magari, pikipiki, baskeli na waenda kwa miguu ilikuwa kila kona ya jiji la Tanga, hakika ni sikukuu kwao.
Mwalimu Salim Mwakalua akiwa katika harakati za kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Wana wa kimji nawo hawakubaki nyuma, huyu mwenye miwani ni mwalimu Zein akiwa na maalim Ubinde.

No comments:

Post a Comment