Monday, June 24, 2013

Rais wa Kenya afanya ziara Uganda wakati nchi yake ina mgomo.

 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesafiri hii leo kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini Uganda. Hii ni ziara ya kwanza ya rais huyo katika nchi jirani ya Uganda tangu kuchukua uongozi wa taifa hilo katika uchaguzi uliofanyika miezi mitatu iliyopita.

Rais Kenyatta anafanya ziara hii kwa mwaliko wa rais Yoweri Museveni ambaye alikuwa Kiongozi wa pekee wa taifa ya nje aliyetoa hotuba katika sherehe ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta, ambapo alikemea mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC kwa kuwalenga viongozi wa Afrika katika oparesheni zake.

Rais Kenyatta na naibu wake wamefunguliwa mashtaka katika mahakama hiyo ya ICC ya kuhusika na machafuko ya baada ya uchaguzi nchini humo mwaka wa 2008.

Rais Museveni ni mmoja wa vingozi wa Afrika wanaopinga mahakama ya ICC akisema kuwa inalenga kuwadhulumu waafrika kauli iliyotolewa na viongozi wa Afrika walipokutana kwenye mkutano wa mataifa ya Afrika au AU mjini Addis Ababa Ethiopia ambpo waliikemea sana mahakama hiyo.

Kwa sasa haijulikani ikiwa swala la ICC litakuwa kwenye ajenda ya mkutanao wa viongozi hao..

Wakati huohuo nchini Kenya kuna taarifa kuwa Chama cha kitaifa cha walimu nchini Kenya, kimetangaza mgomo wa kitaifa kuanzia leo baada ya serikali kukosa kuwalipa marupurupu yao.

Huu ni mgomo wa saba wa walimu tangu mwaka 2007.

Mwnyekiti wa kitaifa wa chama hicho,Wilson Sossion alituhumu serikali kwa kucheza siasa na maswala yanayowahusu walimu kwani wanafahamau masaibu ya walimu na mkataba wa mwaka 1997 uliotoa ahadi ya marupurupu hayo kwa walimu.

Kulingana na makubaliano hayo, serikali inapaswa kuwalipa walimu marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu , kuwlaipia nyumba , matibabu na pesa za usafiri.

"tumedurusu mienendo ya serikali na kugundua kuwa wantumia mtindo wa kugawanya watu. Hilo halitafanya halitafaulu,'' alisema bwana Sossion

"tumetangza kuwa mgomo wa waalimu unaanza rasmi leo, '' aliongeza bwana Sossion

Sossion pia alisema kuwa tume ya kushughulikia maswala ya walimu, haina mamlaka ya kuwaamuru walimu kutogoma au vinginevyo kwani hilo ni jukumu la Knut.

Katibu mkuu Knut, bwana Nyamu aliseama kuwa chama cha walimu kimeweka bayana matakwa yao waliyokubana na serikali mwaka 1997.

"marupurupu haya yote sharti yalipwe.Tumekwenda kwa wizara ya limu ya kuelezea malalmiko yetu,'' alisema bwana Nyamu.

"tunawaambia walimu kuwa katibu mkuu atawapa maagizo kuhusu watakachofanya wakati wa mgomo huu. Walimu waanze kwa kukabidhi majukumu yao katika shule zao leo.

Nyamu pia aliwataka walimu kuwaondoa watoto wao shuleni kwani walimu hawatakuwepo kuwafundisha.

''Kwa sasa tunaiacha serikali ifanye uamuzi , tutaketi chini na kusubiri,'' alisema Nyamu

''Wanachokitaka walimu ni pesa, na wale wanaomshauri rais wamwambie kuwa lazima walimi wapewe pesa kwani hawatazungumzia kingine ila marupurupu yao,'' alisema Sossion.
.
Walimu wakitangaza mgomo, ambao unakuwa mgomo wa tano tangu mwaka 2007.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment