Saturday, June 15, 2013

Kesho ni mechi kali kati ya timu yenye wacheaji bora dhidi ya timu imara: Kim Paulsen.

 Kocha mkuu Kim Paulsen katikati akizungumza na waandishi wa habari, Kulia ni golikipa wa timu ya Taifa na nahodha, Juma Kaseja. Kushoto ni msemaji wa TFF Boni Wambura.

 Kaseja akijibu maswali ya waandishi wa habari mchana huu kuhusiana na mechi ya kesho.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Paulsen amesema kesho timu yake itapambana kufa na kupona kuhakikisha wanaisambaratisha timu bora barani Afrika Ivory Coast.

Mbali na hayo Kim amekiri kuwa Ivory Coast wapo vizuri na wachezaji wake wanajituma katika ligi maarufu barani ulaya, hivyo inafanya Tembo hao kuwa na wachezaji wenye uwezo binafsi lakini akajitapa kikosi chake ni imara.

"Kesho kutakuwa na mechi kubwa sana ni kati ya timu yenye wachezaji wenye juhudi binafsi dhidi ya timu yetu ya tanzania iliyo imara, naam sisi tuna timu imara inayocheza kwa pamoja lakini wenzetu wana wachezaji wazuri wenye uzoefu," alisema Kim.

Kwa upande wake nahodha wa Stars golikipa Juma Kaseja amesema viongozi na watanzania wameshafanya kinachowapasa kwa upande wao, sasa iliyobaki ni wao kudhihirisha umahiri wakiwa uwanjani.

Katika hatua nyingine kocha mkuu wa Ivory Coast Sabri Lamuochi na nahodha wa timu hiyo Didier Zakora walishindwa kufika katika mkutano na waandishi wa habari kutokana na sababu zisizojulikana ila wakadai watazungumza katika uwanja wa taifa baada ya mazoezi saa tisa alasiri.

Kesho Taifa Stars wanashuka dimbani wakiwa na point sita wakisika nafasi ya pili katika kundi C dhidi ya Ivory Coast wanaoongoza kundi wakiwa na point 10.

Hafidh Kido
kidjembe@gmail.com
Dar es Salaam, Tanzania
15 June, 2013

No comments:

Post a Comment