Waziri mkuu nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa wito kwa mahakama ya kikatiba nchini humo kufutilia mbali agizo la rais wa taifa hilo Robert Mugabe kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwezi Julai.
Tsvangirai ameonya kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na hali ya switofahamu iwapo uchaguzi huo utafanyika.
Katika ombi lake waziri huyo anasema kuwa mda uliotolewa kuandaa shughuli ya usajili wa wapiga kura na uteuzi wa wagombea ni mchache mno.
Hata hivyo Tsvangirai hakusema ni lini angependa uchaguzi huo ufanyike.
Tayari uamuzi huo wa Mugabe kuitisha uchaguzi mapema kuliko ilivyotarajiwa, umekashifiwa na viongozi wengine wa mataifa ya Afrika Kusini.
Rais Mugabe alikwenda mahakamani mwezi jana kufuatia shinikizo kutoka kwa muungano wa nchi za Afrika Kusini (SADC) kubana hatua ya kuakhirisha shughuli nzima ya uchaguzi.
Ikiwa Tsvangirai atashinda kesi hii, anasema mahakamana itakuwa imezuia jambo lisilo la kisheria kuweza kutumbukiza nchi katika hali ya switofahamu.
Tsvangirai anataka uchaguzi ufanyike tu baada ya mageuzi ya sheria za uchaguzi ambayo yametokana na katiba mpya.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment