Wednesday, June 19, 2013

Makamu wa Rais Tanzania awapa baraka mabalozi wapya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 19, 2013 kwa ajili ya kumuaga mhe. Makamu. Kutoka Kushoto ni Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani.
Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment