Sunday, June 30, 2013

Mkutano Mkuu wa Coastal Union leo.


Na Oscar Assenga, Tanga


Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hemed Aurora “Mpiganaji”aliliwaambia waandishi wa habari kuwa agenda kuu itakuwa ni kuwajulisha wanachama wao mafanikio yaliyopatikana katika msimu wa ligi kuu uliomalizika na malengo yao katika msimu ujao.

Aurora alisema suala lengine ambalo litazungumza katika mkutano huo ni Katibu Mkuu wao, Kassim El Siagi kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa wanachama wao ambao watahudhuria lengo likiwa ni kuwapa ufahamu kuhusu mambo hayo.

Aliongeza kuwa agenda nyengine ni kuzungumzia maendeleo ya wachezaji wao pamoja na kuweka mikakati ya ya msimu mpya wa ligi katika mwaka 2013-2014 ambapo lengo lao ni kushiriki ligi hiyo kwa mafanikio makubwa zaidi ya ligi iliyopita.

Mwenyekiti huyo alisema wachezaji waliosajiliwa na klabu hiyo wanatarajiwa kuwasili mkoani hapa kuanzia leo na mpaka Julai 3 mwaka huu wachezaji wote waliosajiliwa watakuwa wamekwisha kuwasili kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.


Akizungumzia usajili wao msimu huu, Aurora alisema walichokifanya ni kuziba mapungufu yaliyijitokeza katika mzunguko wa pili wa ligi ili kuweza kukiimarisha lengo likiwa kuleta upinzani na mafanikio msimu ujao.

Chanzo: assengaoscar.blogspot.com

No comments:

Post a Comment