Mkutano mkuu wa CCM umekamilika kwa Mwenyekiti Jakaya Kikwete kuteua watendaji wake wakuu, kikao kilichobakia sasa ni kile kitakachokaa na kujadili juu ya kupitisha majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa Chama kwa nafasi za wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama kwa
mujibu wa Kanuni na Katiba ya CCM, anayo fursa ya kuteua
wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua
wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao
ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe.
Abdulrahaman Kinana .
Baada ya uteuzi huo
Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri
Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
1.
Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
2.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Vuai Ali Vuai.
3.
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
4.
Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
5.
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
6.
Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
Baada ya mapendekezo
hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao
waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri
Kuu ya Taifa.
Pia, Mwenyekiti
akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka
wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na
Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.
kwa safu hii wabaya wa JK
wameangukia pua, maana walioingia katika orodha hii wote ni watu wenye akili
zao na wataongozwa na makamu mwenyekiti Bara ambae ni mwanasiasa mkongwe mwenye
mrengo wa hayati baba wa Taifa Julius Nyerere ambae ni Philip mangula katibu
mkuu wa zamani CCM.
Haya kazi iendelee….
No comments:
Post a Comment