Pichani ni Stempu ya Shirika la Posta Tanzania ambayo imepambwa na Picha ya Mchezaji
Mashuhuri wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania "Taifa Stars",
Ndugu Jella Mtagwa.
Stempu hii ilitolewa na Shirika la Posta la Tanzania Mwaka 1982 na kuzua kizaazaa kikubwasana
kwa kuwa Mchezaji Mwenyewe Jella Mtagwa hakuhusishwa kabisa katika Mchakato
Mzima wa Kutumia Picha yake katika Stempu hizi za Shirika la Posta.
Lakini sakata husika lilitulizwa na viongozi wa kilichokuwa Chama cha Soka nchini (FAT) wakati huo, Saidi El Maamry (mwenyekiti) na Marehemu Patrick Songora (katibu), ambao walimuelewesha Jella Mtagwa kwamba wao ndio waliotoa Idhini ya Picha yake kutumika kwenye Stempu hizo.
Shirika la Posta waliomba kwa chama hicho kiwapatie jina la mchezaji wanayeona anafaa picha yake kuwekwa kwenye stempu kama kivutio na kuitangazaTanzania
kimataifa.
Viongozi hao wawili walimweleza Jella kwamba, waliamua kumpendekeza yeye kwa vile alitoa mchango mkubwa katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars kilichofuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 na pia alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 1981/1982.
Mpaka leo Shirika la PostaTanzania
halijawahi kumlipa Chochote Jella Mtagwa kwa kutumia Picha yake kwenye
Matangazo ya Stempu zao.
Stempu hii ilitolewa na Shirika la Posta la Tanzania Mwaka 1982 na kuzua kizaazaa kikubwa
Lakini sakata husika lilitulizwa na viongozi wa kilichokuwa Chama cha Soka nchini (FAT) wakati huo, Saidi El Maamry (mwenyekiti) na Marehemu Patrick Songora (katibu), ambao walimuelewesha Jella Mtagwa kwamba wao ndio waliotoa Idhini ya Picha yake kutumika kwenye Stempu hizo.
Shirika la Posta waliomba kwa chama hicho kiwapatie jina la mchezaji wanayeona anafaa picha yake kuwekwa kwenye stempu kama kivutio na kuitangaza
Viongozi hao wawili walimweleza Jella kwamba, waliamua kumpendekeza yeye kwa vile alitoa mchango mkubwa katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars kilichofuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 na pia alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 1981/1982.
Mpaka leo Shirika la Posta
Maelezo
zaidi juu ya mwanasoka huyu nguli yanaeleza kuwa alianzia kucheza soka mjini
Morogoro ambapo alinza na klabu ya Nyota morogoro, akacheza Pan African pamoja
na Young African.
Historia
yake inaeleza kuwa ndugu Jella alisoma shule ya msingi Mwembesono ya Morogoro,
na katika mafanikio makubwa ni kuwa beki namba tano wa timu ya Taifa miaka
hiyo.
Kwa
sasa inaelezwa kuwa nguli huyu wa soka anasumbuliwa na maradhi ya kiharusi na
hakuna hata kiongozi mmoja wa soka hata wale ambao alicheza nao soka miaka hiyo
ambao kwa sasa wapo katika nafasi nzuri katika vyama vya soka akiwemo Rais wa
TFF Leodger Tenga, Adolf Richard, Juma Pondamali ‘Mensah’.
Kidojembe
itajitahidi kufanya utafiti zaidi na ikiwezekana kumtafuta nguli huyu na
kufanya nae mahojiano ili kupata taarifa zake zaidi na ikiwezekana blogu hii
imfuate mpaka kwake na kujua anaendelea vipi.
Mtu
yeyote mwenye taarifa za nguli huyu, awasiliane na blogu hii ili tuweze kufika
anapoishi. Shime Watanzania, Tutetee Haki na Maslahi Bora kwa Wachezaji.
Uungwana ni Vitendo.
0713
593894/ 0752 593894
Kwa
taarifa zaidi za namna hii like ukurasa wa ‘watanzania mashuhuri’ ilipopatikana
taarifa hii.
Picha
na Maelezo haya ni Sehemu ya Kampeni ya Ukurasa wa "Watanzania
Mashuhuri"
No comments:
Post a Comment