Na:Na Mussa Juma
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imewaamuru madiwani watano waliotimuliwa Chadema kulipa gharama za kesi waliyokuwa wamefungua kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imewaamuru madiwani watano waliotimuliwa Chadema kulipa gharama za kesi waliyokuwa wamefungua kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Charles Magesa alitoa hukumu hiyo jana baada ya Chadema kushinda kesi
hiyo.Hakimu Magesa alisema madiwani hao wanapaswa kulipa Sh15 milioni ndani ya
miezi miwili, wakishindwa watapelekwa gerezani.
Madiwani hao ni Estomih Mallah
(aliyekuwa Naibu Meya ya Manispaa ya Arusha kipindi hicho), John Bayo aliyekuwa
Diwani wa Elerai, Reuben Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema
Mohamed aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu.
Pia, katika kesi hiyo ya madai
Chadema walikuwa wakiwakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, wakati wadaiwa hao
walikuwa wakijitetea wenyewe baada ya aliyekuwa wakili wao kujitoa.Akisoma
uamuzi huo, Hakimu Magesa alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote,
imeona wadaiwa hao wanapaswa kulipa zaidi ya Sh15.1 milioni, kila mmoja
anatakiwa kulipa zaidi ya Sh3.2 milioni katika kipindi kisichozidi miezi
miwili.
Awali, kulikuwa na mvutano kati ya
wadaiwa hao jambo lililosababisha kesi hiyo kusikilizwa kwa kipindi kirefu
ambapo walitakiwa kueleza mahakama hiyo sababu ya kutokupelekwa gerezani, huku
kila mmoja akitamka kiwango cha fedha ambacho angeweza kulipa kwa mwezi.
Kwa upande wake, Ngowi alisema ana
uwezo wa kulipa Sh25,000 kwa mwezi, Mpanda Sh20,000, Mallah Sh20,000, Rehema
Sh15,000 na Bayo Sh15,000 kwa mwezi bila kuonyesha mchanganuo wa kipato chao, jambo
lililopingwa vikali na Wakili Kimomogoro kwamba kiwango hicho ni kidogo.
Hakimu Magesa alisema kisheria mtu
akishinda kesi ana uwezo wa kuchagua hukumu ya kulipwa kwa kuchukua mali za
mdaiwa au mlalamikiwa kupelekwa kifungoni.
“Kimsingi mtu anaposhinda kesi
lazima alipwe gharama aliyotumia na iwapo mahakama itaridhia alipwe kwa kiwango
hicho, itachukua muda mrefu kati ya miaka 10 na 16 kumaliza deni hilo, jambo
litakalosababisha aliyeshinda kushindwa kuona matunda ya ushindi wake,” alisema
Magesa.
Alisema fedha hizo wanapaswa
kuzilipa mara mbili, awamu ya kwanza inatakiwa kila mmoja kulipa zaidi ya
Sh1.5 milioni na wawe wamemaliza kwa miezi miwili na kwamba, iwapo
watashindwa mdai anaweza kupeleka mchanganuo wa gharama za kumtunza mfungwa na
mahakama kuupitia na baadaye kutoa amri wapelekwe gerezani
No comments:
Post a Comment