Kuna baadhi ya wenyeji wa bara hili waliotegemea mengi
zaidi kutoka kwa mwanawe mtu aliyekuwa akichunga mbuzi huko Magharibi mwa Kenya
Lakini Rais Barack Obama, katika muhula wake wa kwanza,
alizuru Afrika mara moja tu, tena kama mpita
njia, na kusema wazi kwamba hangekuwa anajihusisha kupita kiasi na maswala ya
Afrika.
“Hatima ya Afrika iko mikononi mwa Waafrika
wenyewe,” alisema huko Ghana ,
katika hotuba iliyodhihirisha wazi kwamba ushawishi wa Marekani unapungua
katika bara ambalo sasa linafanya biashara zaidi na Uchina kuliko Marekani.
Kwa
hivyo, ni mabadiliko yapi yatakayokuwepo katika muhula wa pili?
“Kama
Kenya
itafanya uchaguzi huru, basi Obama ataitembelea nchi hiyo.''
Swala
hili la yeye kutokuwa na muda na Afrika, kwa sababu ya matukio mengine,
halikutiwa mkazo katika uchaguzi ulioangazia maswala nyeti nchini Marekani na
harakati za mapinduzi katika nchi za Kiarabu.
Akitoa
hotuba yake baada ya kushinda, Bwana Obama aligusia tu “,muongo wa vita” na
“watu walioko katika nchi za mbali… wanaoweka maisha yao
hatarini ili tu kujadili masuala muhimu, na kupata nafasi, kama sisi, kupiga
kura kama sisi tulivyopiga leo”
Hakuna “Kanuni za Obama”
Katika
muhula wa kwanza, maswala yalilenga mizozo mikubwa iliyokuwa Ivory Coast,
Somalia, Sudan and Sudan Kusini, na hata uchaguzi uliofanywa Zambia.
Kuna
uwezekano kwamba mwanzo wa muhula wa pili atajishughulisha na masuala kama
hayo: mikakati ya kimataifa kuwaondoa waasi wenye uhusiano na Al-Qaeda kutoka Mali kaskazini – kwa kutumia nguvu au
mazungumzo, au yote mawili – na juhudi kuhakikisha kuwa Zimbabwe na Kenya hawatakuwa tena na michafuko
baada ya uchaguzi, iliyoharibu chaguzi zao zilizopita.
Hadi
sasa, hakujawa na ishara yoyote ya kuwepo kwa “Sera Kabambe ya Obama” kwa ajili
ya Afrika. Labda hilo
siyo jambo baya ukitilia maanani tofauti na masuala mengine kuhusu Afrika.
Bwana Obama kawaachia wengine watoe tahadhari
kuhusu Uchina, nchi ambayo haijitoshelezi kirasilimali.
Lakini
kuna uwezekano kwamba muhula wake wa pili utampa nafasi ya kujiondoa kutoka kwa
mkakati wake wa “vita dhidi ya ugaidi” huko Mali
na Somalia , na kuangazia
maswala mapana zaidi – hususan biashara – jambo aliloligusia miaka mitatu
iliyopita nchini Ghana .
Chanzo:BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment