Saturday, November 3, 2012

Release No. 177 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARINovemba 3, 2012

MABADILIKO YA MECHI ZA VPL NAMBA 67,75,79,81 NA 82

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko ya mechi hizo baada ya kutokea dharura, hivyo kushindwa kufanyika kwa mujibu wa kanuni. 

Sababu za mabadiliko hayo ni timu ya Tanzania Prisons kupata ajali wakati ikienda Tanga kwa ajili ya mechi dhidi ya Mgambo Shooting. 

Pia mvua kubwa iliyonyesha jijini Mwanza ilisababisha kutofanyika kwa mechi ya Oktoba 31 mwaka huu kati ya Toto Africans na Kagera Sugar. 

Mechi hizo sasa zitafanyika kama ifuatavyo; Mgambo Shooting vs Tanzania Prisons (14/11/2012- Mkwakwani, Tanga), Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons (18/11/2012- Mabatini, Pwani), Mtibwa Sugar vs JKT Ruvu (7/11/2012- Manungu, Morogoro), Kagera Sugar vs Tanzania Prisons (4/11/2012- Kaitaba, Bukoba), na Ruvu Shooting vs Toto Africans (4/11/2012- Mabatini, Pwani). 

MABADILIKO MADOGO LIGI DARAJA LA KWANZA 

Mechi mbili za Ligi Daraja la Kwanza zimefanyiwa mabadiliko. Mechi kati ya Tessema vs Ndanda iliyokuwa ichezwe tarehe 4/11/2012 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani sasa itafanyika tarehe 5/11/2012 katika uwanja huo huo. 

Mabadiliko hayo yanapisha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting vs Toto Africans ambayo itachezwa 4/11/2012 kwenye uwanja huo huo. 
Ashanti United vs Tessema zilizokuwa zicheze Uwanja wa Mabatini 7/11/2012 sasa zitacheza siku inayofuata (8/11/2012). 
Mabadiliko hayo ni kutoa fursa ya kupumzika kwa Tessema ambayo 5/11/2012 itacheza na Ndanda.

No comments:

Post a Comment