Thursday, November 8, 2012

Kunradh

Ndugu zangu,

Kidojembe ni blogu ya kijamii inayotazamwa na watu wa mataifa mengi. Nilitumia picha za wapenzi waliogandana muda mfupi uliopita. lakini nikapata taarifa kuwa picha hiyo si ya leo, bali ni tukio lililowahi kutokea Kenya mwezi wa tano mwaka huu kwa tukio linalofanana na la leo.

Hivyo kama kuna mtu amepata usumbufu wowote kutokana na picha ile, kidojembe inaomba radhi na tunahakikisha tukio kama hilo halitotokea tena.

Lakini taarifa za tukio ni za kweli, ingawa kama nilivyotangulia kusema awali taarifa zinakanganya maana kila mmoja anazungumza anachokijua. Baada ya taarifa ya habari ya usiku ndipo nitawaletea mzigo mzima.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment