Kuvuta sigara “kunaozesha” ubongo
kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo wa
kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini
Uingereza.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri
wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi
pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Wanasayansi walisema ni sharti watu
wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa
wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na
kiharusi.
Shirikisho la kuhamasisha kuhusu
ugonjwa wa Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema:
"Sote tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu,
kipimo cha Cholesterol au kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri vibaya
moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia vinaathiri ubongo.
"Ni sharti watu wale chakula
chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara,
wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
Kuvuta sigara “kwaozesha” ubongo kwa
kuathiri vibaya kumbukumbu, masomo na uwezo wa kushaurianana, kulingana na
wachunguzi wa King’s College, London.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri
wa zaidi ya miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito uliopita
kiasi pia ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Wanasayansi walisema ni sharti watu
wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi wa King's College
walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya mshtuko wa
moyo na kiharusi.
shirikikisho la kuhamasisha ugonjwa
wa Alzheimer, unaoathiri kumbumkumbu, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba
uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha cholesterol cha juu,
huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia
vinaathiri uongo.
"Ni sharti watu wale chakula
chenye lishe bora, wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara,
wapimwe shinikizo la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
Chanzo: BBC Swahili..
No comments:
Post a Comment