Saturday, November 10, 2012

Taarifa nilizopata ni kuwa Yanga hatoki mkwakwani kesho dhidi ya Coastal Union..

 hiki ni kikosi kazi kikiongozwa na mwenyekiti wa Coastal, Ahmed Hilal 'Aurora' ambacho kitahakikisha yanga anaumiakesho.

 Mwenyekiti akiwa na mwalimu Moroco, leo katika mechi ya Azam dhidi ya Mgambo.. Ambapo Mgambo waliishangaza Tanzania kwa kuichabanga Rambaramba 2-1. Wa kwanza kutoka kushoto mchezaji wa zamani wa coastal Said Kolongo wa nne alievaa kofia ni Ally Kidi mwalimu msaidizi wa Coastal.
 Mwenyekiti wa kamati ya hamasa na ushangiliaji Miraji Wandi, akiwa na mchezaji wa kimataifa wa Kibrazil Gabriel Barbosa. Ambae anaichezea Coastal Union kwa sasa, pembeni ni mkewe na mtoto wake. Katika uwanja wa mkwakwani lao...


 Msemaji wa wa Coastal Edo Kumwembe akitafakari jambo na mwalimu wa Coastal leo uwanja wa Mkwakwani.\
                                                            Barbosa akiingia uwanja...

 Kigoma cha Azam wakati kilipokuwa na ari kabla ya kupunguzwa nguvu na mashambulizi ya Mgambo ambao walionekana kuwadharau...

Miraji Wandi aliposhindwa kujizuia na kuanza kushangilia ushindi wa JKT Mgambo, ambapo ushindi wa Mgambo umeisafishia njia Coastal Union ambayo inasaka nafasi ya pili ili ikamilishe mzunguko wa kwanza kwa mafanikio. Inakumbukwa Coastal ambayo imerudi katika ramani ya soka msimu uliopita, msimu uliopita katika mzunguko wa kwanza kama huu ilimaliza nafasi ya tano katika nafasi ya 13 ikiwa na point 11.

No comments:

Post a Comment