Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia
madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi
hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa,
imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha
kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia
Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo
amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta
kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa
Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao mpia wameutekja mji wa
Sake, lakini msemaji wa serikali Lambert Mende, amesema wanajeshi wa serikali
wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Waasi hao ambao wanaaminika kuungwa
mkono na serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi
mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa rais Joseph Kabila hatabuli kuanzisha mazungumzo ya
amani.
Mazungumzo
ya Amani
Uganda inaandaa mkutano wa marais wa
Rwanda na Uganda hii leo na kuna ripoti kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo
la waasi wa M23 wamesafiri mjini Kampala kushiriki katika mazungumzo hayo.
Ripoti iliyoandikiwa Umoja wa
Mataifa na kundi moja wa wataalamu huru, imesema kuwa Generali Amisi, anaendesha
mtandao wa kusambaza silaha kwa makundi ya kihalifu na waasi wanaohudumu
Mashariki mwa Congo, eneo ambao bado kuna idadi kubwa ya wapiganaji wa waasi.
Hata hivyo kundi hilo la M23
halikuwa miongoni mwa makundi yaliyotajwa kwenye ripoti hiyo lakini kundi la
Raia Mutomboki, moja ya makundi kadhaa yanayojumuisha wapiganaji wa Mai Mai,
inaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na kundi hilo la M23.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa
imenadi kuwa Generali Amisi aliagiza bundi 300, aina ya AK-47 kukabithiwa kundi
moja linalohudumu katika eneo hilo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, lijulikanalo kama Nyatura.
Ripoti hiyo imeongeza kusema kuwa
waasi hao wananunua risasi kutoka kwa nchi jirani ya Congo na kusafirisha
kupitia Kinshasa hado Mashariki mwa nchi hiyo na mtandao unaoendeshwa na
washirika wa Generali Amisi, wakiwemo baadhi ya jamaa ya familia yake.
No comments:
Post a Comment