Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya
Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe
wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha
kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya
mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka
1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini
mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali
za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe
za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais
mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara
baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda
tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi.
picha kwa hisani ya ofisi ya makamu wa Rais.
No comments:
Post a Comment