Wanajeshi wakishika doria katika
makao makuu ya polisi, ambapo mshambuliaji wa kujitoa mhanga alishambulia mwaka
jana
Polisi nchini Nigeri wanasema kuwa
watu wenye silaha wameshambulia kambi ya polisi wa usalama iliyoko katika eneo
lenye ulinzi mkali katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.
Kituo hicho kina jengo la askari wa
kikosi maalum cha kudhibiti wizi - ambapo pia wanashikiliwa wafuasi wa kundi la
kiislamu lenye itikadi kali la , Boko Haram.
Boko haramu linalotaka kuondoa
madarakani serikali ya Nigeria na kuweka sheria kali za kiislamu , limekuwa
likifanya mashambulio kadhaa katika miezi ya hivi karibuni.
Shambulio la hivi karibuni lilikuwa
ni la mabomu mawili ya kujitolea mhanga yaliyolipuliwa jana karibu na kituo cha
kijeshi katika mji wa kaskazini wa Kaduna.
Shambulio hili linakuja siku moja
baada ya mashambulio mawili ya kujitoa mhanga ambapo watu kumi na moja waliuawa
ika kanisa iliyoko ndani ya kambi ya jeshi katika jimbo la Kaduna.
Raia mmoja mjini Abuja anasema
alisikia milio ya risasi kwa takriban nusu saa mapema Jumatatu.
Hata hivyo msemaji wa polisi hakutoa
maelzo ya ziada kuhusu shambulio hilo.
Hata hivyo kwa kuwa jengo hilo lina
ulinzi mkali, hakuna dalili za uharibifu wowote kwa jengo hilo.
Washukiwa wa uhafu pia huziliwa
katika jengo hilo mara kwa mara.
Mwaka jana mshambuliaji wa kujitoa
mhanga wa kundi hilo alishambulia makao makuu ya polisi katika mji mkuu na
kuwaua watu sita.
Chanzo:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment