Ni noti za kwanza za Afrika
Kusini kuwa na uso wa kiongozi mweusi na zinachukua mahala pa noti zilizokuwa
na nyuso za wanyama na picha za viwanda.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma anasema kuwa
noti hizo zilikuwa kama ishara ya shukrani kwa
Mandela.
Bwana
Mandela, mweye umri wa miaka 94, ni mmoja wa watu wanaoenziwa sana duniani baada ya kufungwa jela miaka 27
alipokuwa anapigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Gavana
wa benki kuu Gill Marcus alikuwa wa kwanza kutumia noti hiyo kwa kununua bidhaa
katika duka moja mjini Pretoria .
Alisema
kuwa bwana Mandela ana furaha kuona noti hiyo.
Pia
alielezea kuwa Afrika Kusini hujaribu kila baada ya miaka saba kubadili sarafu
yake ya noti kwa sababu za kiusalama.
Sura
ya Mandela iko upande mmoja wa noti hizo mpya wakati wanyama wakubwa watano
Simba, Kifaru, Chui , Ndovu na Nyati, wakiwa upande wa pili.
Alishinda
tuzo la amani la Nobel mwaka 1993 kwa sababu ya harakati zake dhidi ya utawala
wa ubaguzi wa rangi na kuchaguliwa rais mwaka uliofuata kabla ya kujiondoa
mwenyewe mamlakani baada ya kipindi kimoja tu cha utawala wake.
Akisifika
sana kwa jina
lake "Madiba", amestaafu kutoka kwenye ulingo wa siasa.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment