RAIS Mtaafu wa Afrika Kusini, Thabo
Mbeki amesema Bara la Afrika linapaswa kudhibiti utoroshaji wa rasilimali zake
kwenda nje ya bara hilo, kwani ni moja ya sababu za maisha ya watu wake
kuendelea kuwa duni.
Rais Mbeki alisema jana jijini Dar
es Salaam kuwa taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa rasilimali zenye thamani zaidi
ya Dola za Kimarekani Bilioni 50 hutoroshwa kila mwaka kutoka nchi za Afrika na
kwenda kuwanufaisha watu wengine nje ya bara hilo.
“Taarifa zinaonyesha kuwa rasilimali zenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 50 hutoroshwa kila mwaka kwenda nje ya Afrika, lakini kwa mtizamo wangu mimi ni kwamba thamani halisi inaweza kuwa hata mara mbili (Dola za Kimarekani Bilioni 100) kwa mwaka,”alisema Mbeki.
“Taarifa zinaonyesha kuwa rasilimali zenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 50 hutoroshwa kila mwaka kwenda nje ya Afrika, lakini kwa mtizamo wangu mimi ni kwamba thamani halisi inaweza kuwa hata mara mbili (Dola za Kimarekani Bilioni 100) kwa mwaka,”alisema Mbeki.
Mbeki alikuwa akizungumza kwenye
mjadala kuhusu “uongozi wenye malengo kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika”
ulioandaliwa kwa pamoja baina ya taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) ya hapa
nchini na Mbeki Faoundation ya Afirka Kusini.
Kiongozi huyo alisema utoroshaji wa
rasilimali hizo ni matokeo ya udhahifu katika usimamizi wake, na kwamba lazima
Serikali za Afrika zichukue hatua kudhibiti utoroshaji huo.
Kauli ya Mbeki imekuja wakati
Tanzania ikiwa katika mjadala mkali kuhusu taarifa kwamba baadhi ya vigogo
wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, hivyo kuwapo shinikizo la kutaka
wahusika watajwe na fedha hizo zirejeshwe nchini.
Taarifa hizo ziliibuliwa na mapema
mwaka huu na baadhi ya vyombo vya habari likiwamo Gazeti hili na baadaye
ilibainika kwamba fedha hizo ni mali ya Watanzania 27 wakiwemo wanasiasa na
wafanyabiashara. Gazeti hili pia lilibaini kwamba mmoja wa walioficha fedha
hizo anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).
Katika uchunguzi wake, Mwananchi
imebaini pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania
hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (Karibu Sh300 bilioni) kwa viwango
vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa Dola ya Marekani.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na
kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia
anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine Dola 20 milioni (Sh32
bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni).
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa
No comments:
Post a Comment