Thursday, November 8, 2012

Updates za nyepesinyepesi...Ndugu zangu,

Niliwaambia nitakuwa nawapa taarifa zaidi kila ninapozipata, bado zipo taarifa ambazio zinakanganya kila mmoja anazungumza anachojua yeye.

Ukweli ni kuwa baada ya taarifa ya habari ya usiku ndipo zitapatikana taarifa za uhakika. Lakini nilichosikia ni kuwa huyu mwanaume ndie mume wa mtu, alikwenda katika danguro maeneo ya Temeke kupata huduma. Mke wa huyu bwana ndie aliemuwekea tego mumewe ili anase.

Taarifa zinasema mke wa jamaa ametaka kiasi cha pesa ili amsamehe mumewe, pia zipo taarifa nyingine zinasema mganga wa kienyeji alieitwa na ndugu wa jamaa ndie anaetaka kiasi cha pesa ili awaachanishe.

Katika hospitali ya wilaya Temeke polisi wa kutuliza ghasia ilibidi watumie nguvu za ziada kuwatawanya wananchi kwa kutumia mabomu ya machozi maana kila mtu alitaka kushuhudia kinachoendelea.

Taarifa tulizozipata hivi punde kutoka kwa wanahabari wenzangu ni kuwa watu hao ambao wameshakuwa 'mwili mmoja' kwa sasa wapo Hospitali ya taifa Muhimbili.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi.......

No comments:

Post a Comment