Na: Waandishi Wetu,
Hudumabongo@gmail.com
KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za
mkononi, Tigo imeshikilia usukani wa biashara inayoongoza kwa kero kwa wateja
baada ya kuibuka kuwa mshindi miongoni mwa biashara 31 zenye kero kwa wateja
nchini .
Taarifa hii ni matokeo ya zoezi
linaloendeshwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wenye
lengo la kuboresha sekta binfasi nchini Tanzania hususani huduma kwa wateja.
Nafasi ya pili inashikiliwa na
Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO mkoa wa Dar es Salaam ambao katika
mzunguko wa kwanza ndiyo walishikilia usukani wa kero. Wakiongoza kwa kero ya
kukata umeme bila taarifa kitu kinadaiwa kuwa ni mgao.
Nafasi ya tatu imeendelea
kushikiliwa na Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo
imeendelea kushika nafasi hiyo katika mzunguko wa pili.
Hakukuwa na mabadiliko katika
makundi mengine mfano huduma za usafiri wa anga ambapo mshindi amebakia kuwa ni
Precision Air, huku katika huduma za kibenki zikiendelea kushikiliwa na benki
ya CRDB.
Huduma za ving’amuzi vya kulipia
vyenye kero imeendelea kushikiliwa na Star Times waliopata kura 4 za ziada
ukilinganisha na matokeo ya mzunguko wa kwanza.
Katika mzunguko huu biashara mbili
zaidi ziliingia katika kinyanganyiro hicho ambao ni Kampuni mpya ya huduma za
ndege ya Fast Jet na Dalalada inayofanya safari kati ya Mwenge na Kariakoo
yenye nambari za usajili T 868 BHU.
Haya ni maoni ya wateja wa huduma
hizi yaliyokusanywa kupitia akaunti ya twitter @hudumambayatz na Facebook group
ya HUDUMA BONGO ambapo jumla ya kero 174 ziliwasilishwa na wateja toka mchuano
uanze.
Zoezi la kukusanya maoni haya
linaendelea katika mzunguko wa tatu ambapo kauli mbiu ya ni “Sisi ndio waajiri
wenu , huduma bora ni haki yetu”. Kero katika huduma na bidhaa mbalimbali za
kulipia mfano afya, elimu, usafiri, benki, mawasiliano zinapokelewa na
kutafutiwa suluhisho kwa maendeleo ya taifa letu.
Kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu
wa kura na zoezi hili linavyofanyika tembelea link ifuatayo http://bit.ly/10SARH1
No comments:
Post a Comment