Na
sheilla Sezzy
SERIKALI
ya Uswisi imeitaka Tanzania kuwasilisha kwake majina ya watu wanaotuhumiwa
kuficha mabilioni ya fedha nchini humo, kama sharti la kusaidia uchunguzi dhidi
ya tuhuma hizo.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika
amesema suala la kuwasilisha majina ya watuhumiwa ndilo sharti pekee ambalo
Uswisi wametoa na kwamba ndiyo sababu Serikali imekuwa ikitaka wanaofahamu
majina ya watuhumiwa hao wayataje.
Akizungumza jijini Mwanza juzi, Mkuchika alisema ili kushughulikia sualahilo
ipasavyo, Uswisi imeitaka Tanzania
kuwasilisha majina ya vigogo wanaodaiwa kuficha fedha kwenye benki zake.
Alisema hayo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Muungano wa Taasisi za Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki unaofanyika jijini Mwanza kwa siku mbili kuanzia jana.
Kauli hiyo ya Mkuchika imekuja siku chache baada ya kuwapo kwa taarifa zinazodai kuwa Serikali ya Uswisi imetoa masharti kwaTanzania kuwataja wahusika
walioficha fedha nje kwa majina.
Mbali na masharti hayo,Tanzania
imetakiwa kuithibitishia mamlaka ya Uswisi kuwa mabilioni hayo ya fedha
yametokana na rushwa na nani aliyehonga, uhamishaji wa fedha hizo, jinsi
ulivyofanyika ili Serikali ya Uswisi iweze kutoa ushirikiano kusaidia kuwatia
hatiani watuhumiwa.
Hata hivyo, Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Uswisi kupitia benki zake, imetoa sharti moja tu kwaTanzania katika
kushughulikia suala hilo ;
kutaja majina ya watuhumiwa.
Ingawa Mkuchika hakutaja majina ya watu wanaopaswa kutaja majina ya vigogo hao, aliyewahi kujitokeza na kutoa tuhuma hizo ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Zitto alitoa kauli hizo katika Bunge laTisa wakati akiwakilisha
hoja binafsi na kulitaka Bunge kuchunguza na kuieleza Serikali ili iweze
kuchukua hatua dhidi ya Watanzania walioficha fedha nje ya nchi.
Waziri Mkuchika alisema kuwa tayari Serikali imeishatia mkono wake katika sualahilo kwa kuitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kutafuta ukweli wa jambo hilo
katika benki za Uswisi.
“Baada ya kumwagiza mwanasheria kufanya kazi hiyo alitekeleza na akapatiwa majibu ambayo walitoa sharti moja la kutajwa kwa majina ya vigogo hao ili waweze kuthibitishakama watu hao walificha fedha hizo chafu katika benki
zao,” alisema Mkuchika.
Alisema kuwa benki za Uswisi haziwezi kutaja majina ya wateja wao walioweka fedha huko moja kwa moja kwa sababu ina wateja wengi raia waTanzania ambao wanahifadhi fedha
zao huko.
Mkuchika alisema Serikali yaTanzania
imejijengea tabia ya kuwawajibisha wale wote wanaokiuka sheria za nchi na ndiyo
maana katika kipindi hiki cha Awamu ya Nne sheria ya kupambana na rushwa
ilijadiliwa bungeni na baada ya kuonekana kuwa ina upungufu ikarekebishwa.
Alisema kuwa kutokana na kubadilishwa kwa sheria ya kupambana na rushwa, hivi sasa hata mawaziri na makatibu wakuu wanawajibishwa na kuchukuliwa hatua za kisheria pindi wanapokuwa na makosa mbalimbali hivyo aliye na majina ajitokeze ili wahusika watiwe nguvuni.
Zitto anena
Hoja hiyo ya kutajwa kwa majina ya vigogo walioficha fedha Uswisi ilitokana na kauli ya Zitto hivi karibuni bungeni kuwalipua viongozi waandamizi wa Serikali hii wachunguzwe kutokana na makosa ya kuficha fedha nje ya nchi.
Alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Waziri jana, Zitto alisema: “Bunge limeshaamua na kutoa maelekezo kwa Serikali kufanya uchunguzi kuhusu sualahilo , waziri asibwabwaje mitaani. Anapaswa
kuwa ameanza kazi. Nimeahidi ushirikiano wangu wote.”
Aliendelea: “Nina mchunguzi aliyenisaidia kufanya uchunguzi ambao nitaukabidhi kwa Serikali. Sasahilo siyo suala la Zitto tena, kama
Waziri ana maoni ayatoe bungeni, hivi sasa ni kazi na taarifa. Waziri kusemea
suala hilo nje
ya bunge ni contempt of Parliament,” alisema.
Akizungumza jijini Mwanza juzi, Mkuchika alisema ili kushughulikia suala
Alisema hayo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Muungano wa Taasisi za Kupambana na Rushwa za Afrika Mashariki unaofanyika jijini Mwanza kwa siku mbili kuanzia jana.
Kauli hiyo ya Mkuchika imekuja siku chache baada ya kuwapo kwa taarifa zinazodai kuwa Serikali ya Uswisi imetoa masharti kwa
Mbali na masharti hayo,
Hata hivyo, Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Uswisi kupitia benki zake, imetoa sharti moja tu kwa
Ingawa Mkuchika hakutaja majina ya watu wanaopaswa kutaja majina ya vigogo hao, aliyewahi kujitokeza na kutoa tuhuma hizo ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Zitto alitoa kauli hizo katika Bunge la
Waziri Mkuchika alisema kuwa tayari Serikali imeishatia mkono wake katika suala
“Baada ya kumwagiza mwanasheria kufanya kazi hiyo alitekeleza na akapatiwa majibu ambayo walitoa sharti moja la kutajwa kwa majina ya vigogo hao ili waweze kuthibitisha
Alisema kuwa benki za Uswisi haziwezi kutaja majina ya wateja wao walioweka fedha huko moja kwa moja kwa sababu ina wateja wengi raia wa
Mkuchika alisema Serikali ya
Alisema kuwa kutokana na kubadilishwa kwa sheria ya kupambana na rushwa, hivi sasa hata mawaziri na makatibu wakuu wanawajibishwa na kuchukuliwa hatua za kisheria pindi wanapokuwa na makosa mbalimbali hivyo aliye na majina ajitokeze ili wahusika watiwe nguvuni.
Zitto anena
Hoja hiyo ya kutajwa kwa majina ya vigogo walioficha fedha Uswisi ilitokana na kauli ya Zitto hivi karibuni bungeni kuwalipua viongozi waandamizi wa Serikali hii wachunguzwe kutokana na makosa ya kuficha fedha nje ya nchi.
Alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Waziri jana, Zitto alisema: “Bunge limeshaamua na kutoa maelekezo kwa Serikali kufanya uchunguzi kuhusu suala
Aliendelea: “Nina mchunguzi aliyenisaidia kufanya uchunguzi ambao nitaukabidhi kwa Serikali. Sasa
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment