Tuesday, November 6, 2012

Sheikh Soraga afarijiwa na Rais Kikwete...

 Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadil Soraga akitoka katika Hospitali ya mnazi Mmoja mjini Unguja alikopatiwa matibabu ya awali kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya rufaa Muhimbili leo asubuhi baada ya kumwagiwa tindi kali na mtu asiefahamika asubuhi ya leo katika kiwanja cha mwanakwerekwe mjini Unguja wakati akifanya mazoezi.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akimjulia hali Sheikh Soraga katika Hospitali ya Muhimbili leo.

kidojembe inakusanya taarifa zaidi juu ya tukio hili na itawalete kwa kina kila kinachoendelea. Blogu ya ijamii kidojembe, inamuomba Mwenyezi Mungu amsimamie Sheikh Soraga apone haraka. Amen...


No comments:

Post a Comment