Wednesday, November 14, 2012

Enzi hizooooooo....

              Hapa nikiwa Secondary ya MOA (Mwenge Open Academy) kidato cha tano mwaka 2003.

 Nami nilikuwa kiongozi nikiwa chuo cha uandishi wa Habari TSJ, Rais wa chuo si nafasi ndogo usifanye mchezo.

 Huyu anaezungumza ni Bakari Kimwanga, alikuwa waziri mkuu wangu, nami nikiwa Rais. Kwa sasa ni mwandishi wa gazeti la Mtanzania. Nami nipo Raia Mwema, wa kwanza kutoka kushoto anaitwa Mohammed Omary, alikuwa waziri wa michezo kwa sasa yupo katika idara ya utafiti Muhimbili, wa pili kutoka kushito anaitwa Abdulfatah Murtadha, alikuwa waziri pia kwa sasa ni mtangazaji wa Radio mjini Iringa. Hii ilikuwa mwaka 2008.

Hapa nimewekwa kati na warembo, wa kwanza kutoka chini anaitwa Rehema, kwa sasa yupo katika shirika la ndege Precision air, kati ni mimi jembe, wa mwisho anaitwa Zamzam ni muigizaji katika Bongo Movie kwa sasa. Tulikuwa katika ziara ya kimasomo mjini Morogoro, mwaka 2008 TSJ..

No comments:

Post a Comment