Saturday, November 3, 2012

HandeniNdugu zangu,

Wiki iliyopita nilikuwa Wilayani Handeni mkoa wa tanga katika ziara ya wiki moja juu ya mimba na ndoa za utotoni. Kitu ambacho ndugu Muhingo Rweyemamu mkuu mpya wa wilaya hiyo anapigana nacho kufa na kupona.

Nilipata mualiko huu kutoka kwa ndugu Muhingo ambae alipata kuwa mhariri wnagu mkuu nikiandikia The African na Rai miaka miwili mitatu iliyopita, siku aliyokuja Dar es Salaam nikakutana nae katika idara ya habari Maelezo. Nilizungumza nae kidogo tu kuhusiana na kampeni yake ya ‘Niache Nisome’ akanambia naweza kuenda nikiwa tayari na atanipokea.

Nimeandika haya kama mrejesho wa kuwa kimya kwa wiki nzima, wadau wangu walishaanza kuingia shaka kuwa vipi nimeamua kukata tamaa na shughuli hii ya kuwapa watu habari? Mawe, siwezi kukata tamaa maana hiki ndicho kitu nilichoamua kufanya katika maisha yangu, kuachana na shughuli hii kutasababishwa na umauti.

Sitozungumza mambo mengi kwakuwa safari ile ni ya kiofisi na iligharamiwa na ofisi yangu Raia Mwema, kuandika kila kitu katika blogu yangu ya binafsi ni makosa kiutaratibu.

Hivyo subirini kusoma makala kamili katika gazeti jumatano yoyote kuanzia wiki ijayo. Ila picha sitowafanyia hiyana.

HAFIDH KIDO
HANDENI, TANGA
Kidojembe.blogspot.com
0713 593894/0752 593894


 Nilipofika ofisini tu baada ya utambulisho Mkuu wa Wilaya ndugu Muhingo Rweyemamu alipokea simu juu ya mwalimu mkuu wa shule anaetembea na wanafunzi. Baadae kidogo akapokea ujumbe kuhusu mwanafunzi anaeozeshwa. Hapa akisoma ujumbe huo, hii inatokana na kuweka wazi namba zake kwa wakazi wa vijiji vyote 112 vya wilaya hiyo. Hii ni ripoti ya idadi ya vijana wote wanaopatikana katika wilaya ya Handeni. ripoti inasema kuna vijana 12225, wanawake 4652 na wanaume ni 7573, nilifurahishwa sana maana hakujawahi kufanyika utafiti huo tangu wilaya ya Handeni ianzishwe, hivyo ni kitu kipya katika wilaya hiyo ambapo mkuu huyo ameishikilia nafasi hiyo kwa miezi minne tu na amefikiria kitu kizuri kama hicho. Ripoti hiyo itamsaidia kujua vijana wanataka nini na wana matatizo gani.

 Hapa ananionyesha mradi wa maji wa HTM (Handeni Trunk Main) ulioanzishwa mwaka 1974 lakini mpaka sasa haujakamilika na ameahidi kuukamilisha ndani ya miezi kadhaa ijayo. Tayari ameshaagiza vijana wake wamuandikie ripoti ya tatizo la maji wilayani humo, ripoti imetoka na nimepatiwa nitaiandikia makala.

 Maradi upo hivi ndugu wadau wa kidojembe, Tanzania ina miradi mizuri lakini kuikamilisha ndiyo kazi.

 Hapa ni nyumbani kwake alipofika akakuta muuza samaki akiuza Kambale, na ndiyo ukawa mlo wa siku hiyo.

 Nikaagana nae rasmi kesho yake nikaondoka baada ya kukaa wilayani kwake wiki nzima.

 Nikaamua kupiga picha ili kuudhihirishia umma kuwa nami nilifika wilayani humo, kidojembe haina longolongo.

 Hapa niliamua kusafisha viatu, lakini nikakutana na kabinti ka miaka 13 alie nyuma yangu pichani, anauza ice cream za kiafrika. nikanunua kujikumbusha utotoni, lakini nilipomuuliza maswali mawili matatu nikagundua ana shida kubwa. Alimaliza darasa la saba mwaka jana, mama yake ameshindwa kumpeleka shule kidato cha kwanza na yupo mtaani mwaka mzima bila kusoma. Anaitwa Mwajabu.


Itazame vizuuri picha hii utaona kuna matukio matatu yanafanyika kwa wakati mmoja. Mama akifungua biashara, mtoto akimsaidia wakati alitakiwa awe shule, na pembeni mzee akiwa amebeba mzigo mzito..

 Hapa ni njia panda ya kuelekea Handeni, Tanga, kwa msisi na Dar es Salaam. Ni Mkata, nikaamua kupiga kikombe cha Bibi, ni uji wa mchele mtamu kwelikweli. Ilikuwa ni asubuhi sana kama saa kumi na mbili na nusu nikisubiri gari nielekee Dar es Salaam. Vijana hawa walinisikitisha sana baada ya kuwaona asubuhi yote hii badala ya kuenda shule wanafanya azi ya kubeba mizigo. Mkata hii Handeni.

No comments:

Post a Comment