Thursday, November 8, 2012

Tumuombee Mungu Kevin wa Home Alone... Dawa za kulevya zinamuua..

Huyu ni kijana muigizaji maarufu ambae alianza kutamba miaka ya nyuma akiwa kijana mdogo sana na filamu ya Home Alone. Anaitwa Macaulay Culkin. Alikuwa akitumia jina la Kevin McCallister.

Culkin aliezaliwa August 26, 1980 alianza kuigiza akiwa na miaka minne mwanzoni mwa miaka ya thamanini katika filamu maarufu iliyotikisa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya tisini iitwayo Home Alone.

Kwa sasa kijana huyo ambae alipata mafanikio makubwa katika sanaa ya uigizaji anasumbuliwa na tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kupita kiasi.  Alishapata kukamatwa katika mji wa Oklahoma kutokana na kutumia kiasi cha gramu 17.3 cha bangi na baadhi ya mihadarati mingine hatari kwa afya ya mwanaadamu.

Kwa sasa anaishi maisha mabaya na amepoteza haki zake na mali zake nyingi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kupita kiasi. Tumuombee kijana huyu arudi katika hali yake.

Kijana huyo mwenye miaka 32, mbali ya Home Alone 1&2 alipata kuwika katika Lost in New York, Richie Rich, Uncle Buck, My Girl, The Pagemaster na Party Monster. Mbali ya filamu pia aliwahi kushiriki katika kutengeneza vipande vya video ya wimbo wa nguli wa muziki wa pop Michael Jackson ya Black or White.

Kuonyesha ni muigizaji wa kiwango cha juu Macaulay Culkin alichaguliwa kuwa ni mmoja wa waigizaji wa kiwango cha juu kwa watoto na katika orodha ya VH1 na E! alishika namba mbili, pia akawa miongoni mwa watoto 100 maarufu duniani.  

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
kidojembe@gmail.com

No comments:

Post a Comment