Mwezi huu, Majimbo mawili nchini
marekani yamepiga kura kuhalalisha , kudhibiti na kutoza kodi bangi.
Kutokana na matangazo ya kibiashara
na sheria za kudhibiti ulevi wa bangi wakati madereva wakiwa njiani , basi
tunahoji nini cha mno kinachosubiriwa?
Kura iliyopigwa tarehe sita mwezi
Novemba katika majimbo ya Colorado na Washington, bila shaka iliwatia furaha
watumiaji wa Bangi lakini polisi wengi walilala wakiwa na wasiwasi si haba.
Na hatua hiyo ikaleta karibu
malumbano kati ya majimbo hayo mawili na serikali ya kitaifa, kwani bangi
ingali imeharamishwa chini ya sheria za kitaifa. Lakini kama ilivyo ada, kila
jimbo nchini Marekani liko huru kutunga sheria zake.
Marijuana kama inavyojulikana na
wengi, ni dawa ya kulevya inayotumiwa sana nchini Marekani. Lakini sasa
wataalamu wanasema huu ni mwanzo tu wa kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya ambayo
bado imepigwa marufuku.
“Hiki ni kionjo tu, bado mengi
yatakuja’’ alisema Sanho Tree mkuregenzi mkuu wa mradi kuhusu sera ya
mihadarati.
"Ikiwa majimbo haya mawili
yataendelea na harakati zao za kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya, bila mawingu
kuanguka, basi utakuwa mwanzo mpya kwa uhuru wa kisiasa." Alisema Sanho
Lakini watawala wako macho
"Wakuu wa polisi mjini Colorado
wana wasiwasi kuhusu usalama wa watu kwa ujumla" anasema afisaa mmoja wa
polisi John Jackson
Takriban miaka 80 baada ya Marekani
kufutilia mbali sheria iliyoharamisha pombe, tunajaribu kujibu baadhi ya
maswali ya watu walioelezea hisia mbali mbali kuhusu bangi kuhalalishwa.
Je wauzaji na wakulima wa Bangi
wataendesha vipi matangazo ya kibiashara ya bangi?
Ni haramu kwa watu walio chini ya
umri wa mia 21 kupatikana na bangi huku jimbo la Washington likiharamisha
matangazo a kibiashara ya bangi katika maeneo ya watoto kuchezea .
Kwa watu ambao hawajahi kutumia
bangi , harufu na aina zote za bangi ni sawa tu, wakati inapovutwa athari zake
ni sawa tu, yaani hakuna tofauti kubwa.
Wakati itakapohalalishwa, je
wauzaji/makampuni katika maeneo ya Washington na Colorado yataendesha vipi
biashara zao ili kupata wateja wengi?
“Iwe ni soksi au bangi, kitu cha
kwanza mteja atataka kufanya ni kuangalia muuzaji wa bidhaa ile.’’ Hii ni
kulingana na mtaalamu mmoja wa matangazo ya kibiashara mjini New York.
Anasema kuwa soko la bangi lipo
lakini kama ni kwa vijana wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao tayari
wanaitumia , hakuna ugumu hapo, kwani hawatahitaji matangazo ya kuwashawishi
ili kununua.
Kibarua ni kwa wahafidhina ambao
labda kwa sababu ya maadili, hawavuti bangi. Lakini soko linaweza kuwepo kwa
wataalamu wanaosongwa na mawazo au wapambe wa kiafya na kadhalika.
Muuzaji wa bangi anaweza kubuni
mbinu ya kipekee ya kuuza bangi na kuweza kuifunga kwenye pakiti za kuvutia kwa
rangi na ambazo zina mvuto wa kuwa ghali , labda ndio kitu kitakachoweza
kuwavutia wanunuaji.
Je mwajiri anaweza kukulazimisha
kufanyiwa uchunguzi wa madawa ya kulevya?
Katika jimbo la Colorado, utumiaji
wa Bangi bado unaweza kukuweka mashakani, kwani, sheria hiyo mpya, inawaruhusu
waajiri kuharamisha utumiaji wa bangi miongoni mwa wafanyakazi.
"Hii haishurutishi mageuzi
yoyote,’’ anasema Mason Tvert, mmoja wa wanaharakati wanaotaka matumizi ya
Bangi kudhibitiwa kama ilivyo pombe katika jimbo la Colorado.
Sheria ya taifa nayo haina msimamo
halisi kuhusu swala hili
Lakini uchunguzi uliokuwa unafanyiwa
wafanyafakazi kwenye maofisi umendelea kudidimia. Inahofiwa waajiri katika
majimbo ya Colorado na Washington, sasa watatupilia mbali jukumu la kuhakikisha
wafanyakazi maofisini hawaji kazini wakiwa walevi wa bangi
Uchunguzi mwingi unaofanyiwa watu
kubaini ikiwa wanatumia mihadarati, ni kutokana na dhana kuwa wafanyakazi wengi
wanaotumia madawa hayo, huathiri biashara.
Wafanyakazi wengi wanaopatikana
wakiwa na chembechembe za mihadarati mwilini, wanajulikana kama 'wavutaji wa
bangi wa Jumamosi,' yaani waliovuta bangi mwishoni mwa wiki. Na hivyo hawawezi
kufanya kazi.
Sheria za marekani wakati mmoja
ziliharamisha pombe. Je sheria hizi zinaashiria kuwa nchi hiyo iko tayari
kuhalalisha bangi?
Majimbo mawili nayo tayari yamegusia
uwezekano wa kuwasilisha mswaada wa kuhalalisha Bangi.
Baadhi ya watu hutumia Bangi kama
njia ya kujiliwaza, kujiburudisha au wakiwa waraibu. Wengine wanasisitiza kuwa
Bangi inafaida za kimatibabu.
Nini maoni yako kuhusu swala hili
tete?
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment