Tuesday, November 13, 2012

Pole familia ya mariam Khamis na wana Taarab nchini....

                             Enzi za uhai wake akiimba kwa sauti yake nyororo, bibie mariam Khamis.

                                                        Mh.. akhera kwaenda watu jamani.

Mwanamuziki wa Taarab kutoka kundi la TOT nchini bibie Mariam Khamis amefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Muhimbili muda mchache baada ya kujifungua. Taarifa tulizozipata ni kuwa mtoto alitoka salama lakini ndugu yetu ametutoka kutokana na matatizo ya uzazi kitu ambacho ni tatizo kubwa kwa sasa katika bara la Afrika.

Marehemu mbali ya kundi la TOT Taarab pia aliwahi kuimba katika makundi ya Zanzibar Stars, Five Star na East African Melody. Nyimbo zilizomletea umaarufu ni 'Paka Mapepe', 'Huliwezi bifu', 'ndo basi tena', na 'Raha ya Mapenzi'. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.... Amen..

1 comment:

  1. poleni family ya bi mariam khamisi mungu amuweke mahala pema peponi ameen

    ReplyDelete