Tuesday, January 22, 2013

Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia January Makamba akutana na wafanyakazi wa shirika la simu Tanzania kusikilia kero zao jana.


(Hapa ni kama wanasema: tutawajibu nini hawa jamaa?)

 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Injinia Clarence Ichwekeleza wakati wa Mkutano wa Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam jana.

 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa TTCL,Shaban Mrisho wakisikiliza kwa makini kero mbali mbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam, jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
                                                Makamba akijibu hoja za wafanyakazi hao...

Mh.... hawa jamaa mbona kama wamekata tamaa na majibu ya waziri Makamba? Au jamani ni mimi tu ninaeona hivi...

Pcha kwa hisani ya Mjengwa blog

No comments:

Post a Comment