Pep Guardiola, mwenye umri wa miaka 41, awali ilidhaniwa
angelijiunga na Chelsea, au Manchester
City , zote za Uingereza.
Guardiola
ametia saini mkataba wa miaka mitatu na Bayern Munich, hadi mwaka 2016.
Atachukua madaraka ya Jupp Heynckes, ambaye
ameamua kustaafu.
Siku zake akiwa mchezaji, Guardiola,
aliwahi kuvichezea vilabu vya Barcelona, Brescia, Roma, Al.-Ahli, Dorados na
pia timu ya taifa ya Uhispania.
Alikabidhiwa pia tuzo nyingi akiwa
mchezaji.
Katika kazi ya meneja, amewahi kuchukua
ubingwa wa ligi kuu ya Uhispania, La Liga, mara tatu, ushindi wa Supercopa de
Espana mara tatu, mara mbili kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey, ubingwa mara mbili
wa klabu bingwa barani Ulaya, mara mbili Kombe la Uefa na vile vile mara mbili
ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA kwa upande wa vilabu.
Guardiola, ambaye alizaliwa tarehe 18
Januari, mwaka 1971, Santpedor, Uhispania, tangu kuondoka uwanja wa Nou Camp
mwezi Mei mwaka 2012, amepumzika msimu mzima, baada ya kukiwezesha klabu kupata
jumla ya vikombe 14, ikiwa ni pamoja na ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya
mara mbili.
"Tumefurahi sana tumefanikiwa
kumshawishi mtaalamu wa soka Pep Guardiola kuja Bayern Munich, ambaye vilabu
vingi vikuu vilimtamani na kuwasiliana naye," alieleza mkurugenzi mkuu wa
Bayern, Karl-Heinz Rummenigge.
"Yeye ni kati ya makocha waliofanikiwa
sana duniani, na tuna hakika kwamba sio tu ataiwezesha klabu ya Bayern
kung’ara, lakini hata soka ya Ujerumani kwa jumla."
Bayern kwa hivi sasa inaongoza katika ligi
kuu ya Ujerumani ya Bundesliga, na itapambana na Arsenal ya Uingereza mwezi
ujao, ikiwa ni miongoni mwa timu 16 zilizosalia katika michuano ya klabu bingwa
barani Ulaya.
Heynckes, mwenye umri wa miaka 67, kabla ya
siku kuu ya Krismasi alikuwa ameifahamisha klabu hiyo inayocheza katika ligi
kuu ya Bundesliga kwamba hana nia ya kutia saini mkataba mpya baada ya msimu
huu.
Mkataba wake utakwisha tarehe 30 mwezi wa
Juni, na Guardiola atachukua mahala pake siku itakayofuata.
Chanzo:
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment