KUMB: PPR/13 - 1/1
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU BEI KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA
JUMATANO, TAREHE
2 JANUARI 2013
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji
(EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa
za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 2 Januari 2013.
Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni
muhimu kuzingatia yafuatayo.
|
(a)
Bei
za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa
zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 05 Desemba 2012. Katika
toleo hili, bei za rejareja kwa Petroli,
Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa
viwango vifuatavyo: Petroli Sh 126/lita sawa na asilimia 5.96; Dizeli Sh 32/lita
sawa na asilimia 1.60; na Mafuta ya Taa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.50. Bei
za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: Petroli kwa Sh
126.10/lita sawa na asilimia 6.17; Dizeli kwa Sh 32.48/lita sawa na asilimia 1.69;
na Mafuta ya Taa kwa Sh 50.74/lita sawa na asilimia 2.6. Mabadiliko haya ya bei
yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika
kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.
(b)
Kwa
mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli
zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa
taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la
kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
(c)
Kampuni za mafuta zipo huru
kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko
chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na EWURA na
ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la tarehe 23 Desemba 2011.
(d)
Vituo
vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango
yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya
biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana
kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo
vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya
bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
(e)
Wanunuzi
wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la
kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo
ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi
wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu
kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora
kisichofaa.
A: BEI ZA REJAREJA
B: BEI ZA JUMLA
Haruna
Masebu
MKURUGENZI
MKUU
EWURA
|
No comments:
Post a Comment