John Mnyika Mbunge wa Ubungo na waziri kivuli Nishati na madini.
Maelezo kuhusu maamuzi
ya Baraza Kuu nimeyaambatanisha. Lakini pia unaweza kunukuu kutoka majibu ya
nyongeza niliyoyatoa mbele ya wanahabari leo tarehe 29 Januari 2013 wakati wa
mazungumzo yangu nje ya maelezo niliyoyambatanisha kutokana na habari za leo kuwa
CCM kupitia kwa Kinana na Nape imesema kwamba madai ya wananchi wa Mtwara ni ya
msingi.
Kinana hana uhalali wa
kuwatetea wananchi kuhusu gesi kwa kuwa yenye ni mmoja watuhumiwa wa
kuwakosesha wananchi wa Mtwara manufaa ya Gesi, alikuwa alikuwa ni sehemu ya
uongozi wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Artumas na alishiriki kuwakosesha
wananchi wa Mtwara fursa ya umeme wa MW 300 zilizopaswa kuzalishwa Mnazi Bay
toka mwaka 2009. Hatua ambayo kama ingefanyika toka wakati huo mgogoro wa gesi
usingekuwa kwa kiwango cha sasa. Kinana badala ya kujifanya kuwatetea wananchi
wa Mtwara awaeleze alilipwa kiasi gani na kampuni hiyo na kwanini hakutetea
maslahi ya wananchi toka wakati huo.
Kinana na Nape
wazingatie kuwa CCM haina uhalali wa kuwatetea wananchi wa Mtwara kwa kuwa
mgogoro huo ni matokeo ya sera bomu na uongozi mbovu chini ya chama hicho ambao
umeruhusu ufisadi katika sekta hiyo na kukosesha wananchi manufaa ya gesi hiyo katika miradi ya toka
mwaka 2004 hali ambayo imefanya wananchi kuandamana kutaka manufaa ya sasa.
Kinana na Nape badala ya kuisukumia Serikali mzigo wa kwenda kukutana na
wananchi, CCM ijieleze ni kwa nini kwa miaka mingi imetoa ahadi za uongo kuhusu
uendelezaji wa miradi ya gesi kwa wananchi wa Lindi na Mtwara na pia sababu za
kushindwa kuisimamia Serikali kutekeleza miradi ya gesi na umeme Mtwara ikiwemo
wa MW 300 wa Mnazi Bay.
Kauli za Kinana na Nape
kuhusu gesi Mtwara ni za kinafiki kwa kuwa msimamo wa Serikali na CCM
ulishatolewa na Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa kuyapinga madai
hayo ya wananchi. Kikwete alizungumzia
hayo kwenye hotuba yake kwa taifa tarehe 31 Disemba 2012 na kuyapinga
tena katika kauli zake mwezi Januari mwaka 2013.
Mara baada ya Kikwete
kuyakataa madai ya wananchi, wananchi waliendelea kuwa na msimamo na wengine
wakitaka kupata msimamo wa CCM sio wa Serikali na hatimaye mwanzoni mwa mwezi
Januari 2013 Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula alisema CCM haikubaliani
na madai ya wananchi na akawaita wanaCCM wachache na wananchi wengi wenye madai
hayo kuwa ni ‘waasi’.
Hivyo, Kinana na Nape
ambao sio wasemaji wakuu wasitoe kauli za kinafiki za kujikosha baada ya kauli
za Rais Kikwete, Mangula na viongozi
wengine wa CCM na Serikali kuchochea vurugu.
Kauli za kujikosha za
Kinana na Nape haziwezi kurudisha nyuma vuguvugu la wananchi kufanya mabadiliko
kwa kuiondoa CCM madarakani kupitia chaguzi za mwaka 2014 na 2015 na kuiunga
mkono CHADEMA katika mwaka 2013 na kuendelea kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele
kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za taifa pamoja na kuwa na sera sahihi zenye kuwezesha
maendeleo endelevu ya wananchi na nchi kwa ujumla.
John Mnyika (Mb)
No comments:
Post a Comment