Shirikisho la soka la Zambia, linasema linataka shirikisho
la soka duniani FIFA kutambua mcheza soka wa nchi hiyo Godfrey Chitalu kwa
uhodari wake wa kuingiza mabao 107 mnamo mwaka 1972.
Hatua hii inakuja baada ya gwiji wa soka Lionel Messi kuvunja
rekodi ya mcheza soka mjerumani Gerd Mueller aliyeingiza mabao 85 katika mwaka
mmoja. Messi sasa ameingiza mabao 88 mwaka huu (mwaka jana) pekee.
Msemaji wa shirikisho la soka la Zambia, Faz,
Eric Mwanza, aliambia BBC kuwa wana rekodi za kuthibitisha kuwa Chitalu
anapaswa kutambuliwa kwa mabao aliyoingiza.
''Tunataka
kusema wazi kuwa sio swala la kuthibitisha madai yetu au kujaribi kuhakikisha
kuwa ni kweli aliingiza mabao hayo, hakuna utata kuhusu hili.'' alisisitiza
bwana Mwanza.
Kile
ambacho tunahoji hapa ni kwa nini hajatambuliwa na hicho ndicho sisi tunataka''
"tunamtumia
ujumbe, katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, kuangalia upya swala hili la Godfrey
Chitalu."
Baada
ya maisha yake kama mchezaji wa soka, Chitalu alichukua wadhifa wa kocha na
hivyo kuanzisha timu ya taifa ya Zambia .
Alifariki pamoja na wachezaji wengine 29, 18
miongoni mwao wakiwa wachezaji wa kimataifa, katika ajali ya ndege katika pwani
ya Gabon walipokuwa
wanakwenda Senegal
kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia.
Mwanza
pia aliongeza kuwa mwaka 1972, haikuwa ndio mara ya kwanza kwa Chitalu kucheza
vizuri kabisa.
"katika
msimu wa ligi kabla ya mwaka 1972, aliingiza mabao 89 ," bwana Mwanza
alielezea zaidi.
Mnamo
mwaka 1972, aliingiza mabao 107, yaliyohusisha mechi za ligi , mechi za vilabu
, mechi za kitaifa pamoja na mechi za kirafiki''
Rais
wa Faz, Kalusha Bwalya, alisema kuwa anakumbuka vyema sana alivyocheza bwana Chitalu.
''Kwa
hivyo ingekuwa muhimu sana
kumtambua kwa umahiri wake wa kuingiza mabao,'' alisema Bwalya
"baadhi
yetu tumeona wachezaji kama Pele, Platini, Maradona na Van Basten, kama chezaji
wa zamani wa soka, siku hizi, ni vigumu sana kuingiza mabao 20, kwa hivyo
asalie kusifiwa Messi.
Mtandao
mmoja wa nchini Zambia
unadai kuwa Chitalu aliingiza mabao 116 mwaka 1972, lakini haijazingatia mabao
tisa ya kwanza aliyoingiza katika mechi za kilabu bingwa Afrika
Chanzo: BBC Swahili…
No comments:
Post a Comment