Tuesday, January 1, 2013

Juma Sadick Kilowoko Sajuki amefariki dunia....


Hii ni mwishoni mwa mwaka jana alipokuwa jijini Arusha katika sherehe za bongo Movie baada ya kuanguka jukwaani wakati akijitambulisha kwa mashabiki wake wa mji huo.

kwa mujibu wa Gerald Hando mtangazaji wa Radio Clouds Sajuki amefariki alfajiri ya kuamkia leo katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Sajuki amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi yanayasababishwa na viungo vya ndani yaani figo, ini na moyo, alikwenda kutibiwa India lakini hali yake haikuweza kutengemaa...

taarifa nyingine za mahala msiba utakapokuwepo na siku ya maziko zitatolewa hapahapa katika blog yenu baada ya kupata taarifa zaidi kutoka kwa wahusika.

kidojembe inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na mashabiki wa bongo movie kwa msuba huu...
sote ni waja wa MwenyeziMungu na sote tutarejea kwake.
HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment