Bunge la venezuela
limepiga kura ya kuidhinisha kuhakhirishwa kwa shughuli ya kuapishwa kwa raisi
wa venezuela
Hugo Chavez kutawala kwa muhula mpya.
Sherehe hizo zilitarajiwa kufanyika hapo keshio siku ya
Alhamisi.
Manaibu walipiga kura kumpa rais muda
anaohitaji kuweza kupata nafuu kutokana na upasuaji aliofanyiwa wa saratani
mwezi jana.
Makamu
wa raisi Nicolas Maduro amesema kuwa rais Chavez hatoweza kusafiri hadi Venezuela kwa sherehe hiyo ya kuapishwa kutokana
na madakatari wake nchini Cuba
kusema kuwa haruhusiwi kusafiri .
Upinzani
unasema kuwa Bwana Chavez anapaswa kusemekana kuwa hawezi kazi tena na hivyo
spika wa bunge kuchukua nafasi ya rais wa mpito.
Bwana
Chavez, ambaye amakuea mamlakani tangu mwaka 1999, alichaguliwa kwa muhula wake
wa nne mamlakani katika uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment