MWENYEKITI wa Baraza la Wadhamini la Bakwata, Masoud Ikome (72),
amemkana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shekhe Ponda Issa
Ponda, mshirika wake, Shekhe Mukadam Abdallah Swalehe (45) na wafuasi wao kuwa
hawatambui hata kwa sura.
Shekhe Ponda, ambaye ni mwanaharakati maafuru wa kutetea kile anachokiita haki na
Ikome ambaye ni shahidi wa nne wa upande wa mashtaka, jana alikana kumfahamu Shekhe Ponda na wafuasi wake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Hatua hiyo ilikuja baada ya kuambiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka awaangalie washtakiwa hao kwa jumla
“Hata mmoja simtambui na hakuna hata mmoja aliyewahi kuwa mjumbe wa Baraza la Maulamaa,” alidai Ikome.
Ikome alidai kuwa amekuwa akifanya kazi Bakwata tangu Mei 15 mwaka 2010 na kwamba majukumu yake ni kudhibiti mali za Bakwata zinazohamishika na zile zisizohamishika.
Alizitaja
Alidai kuwa mamlaka ya utendaji kazi huo anayapata kutoka, katika Baraza la Maulamaa na kwamba anakifahamu kiwanja namba 311/32 kwa sababu aliwahi kuitisha kikao kupitia Baraza la Wadhamini na kukijadili kuhusu kubadilishwa na kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd huko Kisarawe mkoani Pwani.
“Mabadilishano hayo yalikuwa yana lengo la kupata kiwanja kikubwa ambacho kingeweza kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu. Tulipata ekari 40 zilizokwishapimwa huko Kisarawe ambapo tulibadilishana na ekari nne za Malkazi Chang’ombe.” alisema shahidi huyo.
Alisisitiza kuwa nguvu ya kufanya mabadilishano ya kiwanja cha ekari nne na ekari 40 walizipata kutoka katika Baraza la Maulamaa ambalo lilikaa na kuamua kibadilishwe na kwamba hayo yalifanyika Januari 24.
Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alidai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maulamaa ndiyo katibu wa Baraza la wadhamini Bakwata, Suleiman Said, hivyo habari za utekelezaji wa mabadilishano hayo walikuwa wakizipata kutoka kwake.
Alibainisha kuwa kwa sasa eneo la Chang’ombe Malkazi, linamilikiwa kihalali na Kampuni ya Agritanza Ltd baada ya kukamilishwa kwa taratibu zote za mabadilishano hayo.
Kwa upande wake shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Hafidhi Othman (42), alidai kuwa aliwahi kukutana na Shekhe Ponda ambaye ana mgogoro na Bakwata wa muda mrefu.
Alidai kuwa katika mazungumzo yake na Ponda alimweleza kuwa walichokifanya siyo sahihi kwa sababu wao kama Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Shahidi huyo, anadaiwa kuwa baada ya kuambiwa hivyo na Shekhe Ponda, alimweleza kuwa
Alidai kuwa Shekhe Ponda alikwenda na mzee mmoja ambaye alisema ana eneo la ekari 30 huko Mkuranga ambapo Ponda alimwambia kuwa “Tuache tukaangalie tutakujibu mwishoni mwa wiki na lakini usijenge ukuta.”
Hafidhi alidai kuwa ilipofika Alhamisi alipata habari kuwa Ponda na wafuasi wake watakwenda kuvamia, baada ya kupata taarifa hiyo.
Alidai kuwa ilipofika siku ya Ijumaa baada ya swala nilipita katika eneo
Aliongeza kudai kuwa alikwenda katika kituo cha Polisi cha Kati kutoa taarifa juu ya tukio
Alidai kuwa katika eneo
Pia shahidi huyo alibainisha kuwa fedha zilizotumika kununua ekari 40 za Kisarawe zilitolewa na Kampuni mama ya Agritanza Ltd, Kampuni ya Ali Hillary Ltd.
Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la
Polisi (DCI), Robert Manumba bado ni tete na jana Rais Jakaya Kikwete alikwenda
tena ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam alikolazwa
katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), kumjulia hali.
Chanzo: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment