Wednesday, January 9, 2013

Zanzibar kujenga nyumba za watalii chini ya maji....

 Chumba kinachotarajiwa kuwekwa chini ya Bahari kikiendelea na ujenzi kwenye Hoteli ya Manta Resort Makangale iliyoko Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni hatua kubwa zaidi ya kuimarisha utalii hapa nchini kwa kuvutia watalii wenye matumizi ya juu zaidi ya fedha (daraja la kwanza), ambapo ujenzi wa Chumba hicho kitakacho kuwepo chini ya bahari utagharimu Tsh758,000,000/-za kitanzania.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishusha Nanga kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chumba cha chini ya bahari katika Hoteli ya Manta Resort iliyoko Makangale Kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba, na kuweka historia katika Sekta ya Utalii nchini.

Chanzo: Said powa blog...

No comments:

Post a Comment