ABIRIA mmoja amefariki papohapo huku akiwa na zaidi ya Sh13
milioni mfukoni, wengine 48 wamejeruhiwa mkoani Mbeya baada ya basi walilokuwa
wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Wakati ajali hiyo ikitokea Mbeya, Dar es Salaam watu wawili wamefariki dunia
baada ya mabasi ya daladala kugongana maeneo ya Kongowe, nje kidogo ya Dar es
Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema ajali
hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa magari hayo yaliyokuwa yanashindana.
Majeruhi 12 walipelekwa Hospitali za
Temeke na Muhimbili kwa matibabu.
Katika ajali ya Mbeya, basihilo ambalo ni mali ya Kampuni
ya Nganga Express ilitokea jana asubuhi eneo la Inyala, Wilaya ya Mbeya
Vijijini.
Basihilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam .
Katika ajali ya Mbeya, basi
Basi
Dereva wa basi hilo , Alex
Bunyinyiga alisema wakati akiendesha basi hilo ,
alipofika kwenye mteremko wa Inyara, mahali ambapo kuna kona kali, aliona lori
lililokuwa limeegeshwa upande wa kulia wa barabara.
Bunyinyiga alisema alipolikaribia lori hilo , ghafla lilitokea gari lingine aina ya
Fuso ambalo lilipita lori lililoegeshwa na kumfuata upande wake, hali ambayo
ingesababisha kugongana uso kwa uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alimtaja mtu
aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Enock Lwila, mkazi wa Mama John,
mjini Mbeya.
Diwani alisema Lwila wakati akipatwa na ajali alikuwa na
Sh13 milioni mfukoni ambazo ziliokolewa na polisi waliowahi eneo la
tukio. Diwani alisema kwa sasa fedha hizo ziko salama mikononi mwa
polisi na kwamba, baada ya kupatikana nduguwatakabidhiwa.
No comments:
Post a Comment