Aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor ambaye amezuiliwa
kwa makosa ya jinai, amewaandikia barua wabunge wa nchi hiyo na kuwataka
wamlipe malipo yake ya uzeeni dola 25,000.
Katibu wa baraza la senate, Nanborloh Singbeh amesema kuwa
barua hiyo itaweza kujadiliwa na wabunge katika kikao cha wiki ijayo.
Barua hiyo inayosemekana kutoka kwa Taylor inasema kuwa kubana
malipo yake ya uzeeni ni dhulma kubwa kwake.
Mwezi
Mei mwaka jana, mahakama iliyokuwa inasikiliza kesi za ukiukwaji wa haki za
binadamu nchini Sierra Leone ,
ilimhukumu Taylor
miaka 50 gerezani kwa makosa 11 ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hata
hivyo Taylor , amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo
iliyotolewa na mahakama maalum ya Sierra Leone iliyoungwa mkono na
Umoja wa Mataifa.
Iliamua
kuwa Taylor , aliunga mkono waasi waliofanya uasi
nchini Sierra Leone
wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991-2002.
Mwandishi wa BBC Jonathan Paye-Layleh mjini Monrovia anasema kuwa saini iliyo kwenye barua hiyo
inafanana sana na ile ya bwana Taylor .
Hata
hivyo, imebainika kuwa barua hiyo ina makosa kadhaa ya kisarufi,
Kilio
cha Taylor kimesababisha maswali kuhusu ikiwa Taylor ndiye aliandika
barua hiyo.
Hata
hivyo, shemeji yake Taylor Arthur Saye aliambia waandishi wa habari kuwa rais
huyo wa zamani ndiye aliandika barua hiyo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment