Monday, January 14, 2013

Rais wa TFF Leodger Tenga aaga rasmi...

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Leodger Ochila Tenga ametangaza rasmi kuwa hatogombea nafasi hiyo katika uchaguzi unaotegemewa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho hilo jijini Dar es Salaam leo mchana, Tenga ambae aliliongoza shirikisho hilo kwa vipindi viwili yaani miaka minane sasa, mbali ya katiba kumruhusu kugombea kwa mara ya tatu lakini yeye amesema huu ni wakati wake kukaa pembeni na kupisha watu wengine watakaomalizia alipoishia.

Kidojembe inampongeza Tenga kwa uamuzi huo wa busara na kizalendo.

No comments:

Post a Comment