Tazama jengo lilivyo zuri kwa ndani...
Jengo lilivyoanguka upande wa nyuma... ilipo ngome kongwe.
Hili jahazi liliwekwa mnamo mwaka 2003 katika ukumbi wa chini.
Ukienda Zanzibar wakati
unakaribia gati ya bandari Malindi, kitu cha kwanza kukiona ni jengo zuri la
kizamani liitwalo Bait Al Ajab, ama kwa Kiswahili jumba la maajabu. Kwa namna
nyingine jumba hilo
ndiyo sura ya mji wa Unguja.
Jengo hilo sababu ya kuitwa la maajabu ni uzuri,
ukubwa na samani za gharama kubwa zilizowekwa ndani yake katika miaka ambayo
Afrika bado ilikuwa nyuma kimaendeleo. Vitu viwili ambavyo viliwekwa ndani ya
jumba hilo
ndivyo vya kwanza kutumika katika Afrika Mashariki na kati na kusini mwa jangwa
la sahara.
Umeme na lift vilianza
kutumika Zanzibar mwanzoni mwa karne ya 18,
wakati huo nchi za ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara, ni sehemu ya kwanza
kuwekwa ni katika jumba hilo .
Kwa namna moja ama nyingine hilo linaweza kuwa jengo
la kujivunia kuwa urithi kwa nchi ya Tanzania na kuhitaji kulindwa ama
kuhifadhiwa kwa kiwango kikubwa.
Cha kushangaza mwezi Disemba
tarehe 31 mwaka jana wakati wa sala ya magharibi upande wa nyuma wa jengo lilianguka
kuanzia ghorofa ya pili mpaka sakafuni. Ukumbi mzima wa nyuma ulianguka
kufuatia kuvuja kwa choo kilichokuwa ghorofa ya pili hivyo udongo kunyonya maji
na kushindwa kuhimili uzito wa jengo.
Jengo hilo
ambalo lipo chini ya urithi wa dunia na shirika la UNESCO linatambua uwepo
wake, lilijengwa mwaka 1883 na sultani wa tatu wa Zanzibar alieitwa Sultan Baraghash Bin Said
Bin Sultan kwa matumizi ya starehe na sherehe za kifalme.
Kidojembe ilipata wasaa wa
kuzungumza na Ramadhan Ali Machano ambae
ni mkuu wa huduma za elimu katika jengo hilo na kuweka wazi “Jengo hili
lilijengwa na sultan Baraghash, na alilitumia kwa starehe tu. Kama unavyoona
jumba zima halina jiko wala chumba cha kulala, kote humo ni ‘ma-hall’ (kumbi),
alikuwa akitumia kufanyia sherehe kama maulidi
ama sikukuu na ngoma zao za asili.”
Wakati Afrika ikiwa inaitwa
bara la giza kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo jumba la Bait Al Ajab liliwekwa
umeme mwaka 1886, kufikia mwaka 1913
Zanzibar ikiwa chini ya Waingereza wakati huo Sultan wa kumi akiitwa Sultan
Khalifa Bin Haroub akiongoza ndipo jumba hilo lilipowekwa lift. Ambapo kwa
mujibu wa watu wa historia kwa nchi za Afrika mashariki na kati kusini mwa
jangwa la sahara Zanzibar ndiyo ilikuwa ya kwanza
kutumia lift katika majumba hilo .
Hata hivyo kutokana na husda
ya waingereza mnamo tarehe 27 August, 1896 vilipiganwa vita vifupi kulivyo
vyote duniani ambavyo vilidumu kwa dakika 45 maarufu vita vya Alhamis. Vilisababishwa
na waingereza kulazimisha kuwekwa kwa Sultan wanaemtaka ambae waliamini
atawasaidia kulinda maslahi yao .
Ni baada ya kufariki kwa
Sultan wa sita wa Zanzibar
alieitwa Sultan Hemed Bin Thurein Bin Said. Hivyo miongoni mwa wajukuu wakawa
wanagombania kurithi kiti hicho, lakini miongoni mwa wajukuu hao mmoja
alionekana ana msimamo mkali hivyo waingereza hawakumtaka. Kwa kutumia ujanja
mjukuu huyo alijitangazia ufalme hata kabla babu yake kuzikwa.
Akiwa katika jumba lililojulikana kama
Bait Al Hukmu ‘kwa sasa halipo’ lilikuwa jumba la tatu kutoka jumba la Bait Al
Ajaib. Ndimo mjukuu huyo alipokaa na kusema hawezi kutoka mpaka waingereza
watakapomtambua kuwa yeye ndie mfalme. Waingereza wakampa siku tatu kutoka na
kuondoka Zanzibar , lakini kufikia siku ya tatu
waingereza wakaleta meli za kivita karibu na bandari ya Zanzibar ‘ilipo bustani ya forodhani kwa sasa’
wakaanza kupiga mizinga eneo lote la forodhani mpaka kuharibu bandari yote. Ndipo
waingereza wakajenga bandari mpya eneo la Malindi, ndipo ilipo bandari ya sasa.
Jumba la Bait Al Ajab
lilinusurika kuvunjwa kwasababu mbele yake kulikuwa na mnara mkubwa ambao
ulibomoka kiasi kutokana na makombora yaliyokuwa yakielekezwa katika jumba hilo . Lakini ni sehemu
ndogo eneo la mbele lilivunjika kutokana na makombora hayo.
Kuna uvumi ambao ulivumishwa
na watu kuwa katika nguzo hizo kuna vichwa vya watumwa wa kiafrika viliwekwa
ikiwa ni kafara, lakini bwana Machano alipinga kwa maelezo kuwa mkandarasi wa
jengo hilo alikuwa ni Mwingereza kutoka Scotland .
Mwingereza huyo ambae
hakufahamika jina lake
inadaiwa alikuwa mhandisi
wa meli lakini alikuwa na taaluma ya usanifu majumba. Kwakuwa Waingereza
walikuwa mbele katika kupinga ukatili na kukomesha biashara ya utumwa
hawangeweza kuwa wa kwanza kukata vichwa vya watumwa na kuviweka katika nguzo
hizo.
Kitu cha pili kuupinga uongo
huo kidojembe ilishuhudia kwa macho yake upande ambao jumba hili lilianguka
nguzo nne zilikuwa chini hakukuwa na mafuvu wala mifupa ya binaadam.
Aidha kitu cha kuleta
matumainiSerikali imeunda tume ya watu watano ili kufuatilia gharama
zitakazotumika kukarabati jengo hilo .
Kidojembe ilipata nafasi
kuzungumza na muuza bidhaa za asili kwa watalii bwana Farouq Abdallah ambae
alisema ana mwezi mzima tangu jengo hilo
lianguke hajauza hata kifaa kimoja.
“Tangu jengo hili lifungwe
rasmi mwezi uliopita sijauza hata kifaa kimoja, wazungu hawaji tena maana kwa
siku kulikuwa kunajaa wazungu utadhani kuna arusi ama msiba. Lakini kwa sasa kama unavyoona hakuna mtu hata mmoja jengo limefungwa,
mtihani mtupu.”
Kidojembe ilipanga kuenda
kukutana na waziri mwenye dhamana ya masuala ya utamaduni lakini haikupata
nafasi kwani viongozi wote wa kiserikali walikuwa katika maandalizi ya sherehe
za mapinduzi. Lakini blog yako inakuahidi kulifuatilia suala hilo ili kujua mwisho wake.
HAFIDH KIDO
0713 593894
10/1/2013
Unguja, Zanzibar
No comments:
Post a Comment