Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ghana Kwesi Appiah,
amemuondoa Andre 'Dede' Ayew katika kikosi chake kitakacho shiriki katika
michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Ayew,
alikosa kufika kambini Abu Dhab kutokana na jeraha la paja, ambalo bado
halijathibitishwa na madaktari wa timu hiyo.
Mcheza
kiungo huyo aliruhusiwa na klabu yake ya Ufaransa ya Marseille, ili ajiunge na
timu hiyo ya taifa ya Ghana ,
kufuatia ombi lililowasilishwa kwa klabu hiyo na shirikisho la mchezo huo
nchini Ghana .
'' Nimeamua kumuacha nje ya kikosi changu kitakacho elekea
Afrika Kusini'' Alisema Appiah.
Chini ya sheria za FIFA, vilabu vya soka
vinapaswa kuwaruhusu wachezaji siku ya Jumamosi, wiki mbili kabla ya kuanza kwa
fainali hizo za Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini.
Vilabu
pia ni shartiw aruhusu wachezaji waliojeruhiwa kuchunguzwa na madaktari wa timu
zao za taifa.
''Andre hakujitokeza, licha ya kuwa tayari alikuwa amepewa
idhini na klabu yake na pia kukabithiwa tikiti ya ndege ya shirikisho la mchezo
wa soka la Ghana ,
ili asafiri kutoka Ufaransa hadi kambini'' Kocha huyo aliongeza.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa ni jambo
la kusikitisha kuwa hakufika kambini na kusema kwamba hakuwa amemaliza matibabu
aliyokuwa akipewa na daktari wake ili afike kambini siku ya Jumatano, tarehe 9
mwezi huu.
''Mchezaji
huyo aliamriwa kufika kambini siku ya Jumatatu kwa kuwas siku ya Jumatano ndio
siku ya mwisho kwa nchi mbali mbali kuwasilisha majina ya wachezaji wake kwa
shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF.
Appiah
kwa sasa ana kikosi cha wachezaji 25 na ni sharti apunguze kikosi hicho kabla
ya siku ya Jumatano, wakati atakapotaja rasmi kikosi kitakacho akilisha Ghana kwenye
faianli hizo.
No comments:
Post a Comment