Thursday, January 10, 2013

Azam watinga fainali na kuwagaragaza Simba B kombe la Mapinduzi Zanzibar...

 Mkipalamoto kushoto akikabiliana na David Mwantika wa Azam jana usiku... Azam waliingia fainali kwa mikwaju ya penalt 5-4.

 Jamani Gaudience Mwaikimba amerudi mpya kama alivyokuwa Yanga. Nilikutana na Mwaikimba katika uwanja wa Kaitaba mwaka juzi alipokuwa Kagera Sugar, nikasema Mwaikimba kwisha habari yake... Hapa alishindwa kufunga bao hili ila alionyesha uwezo mkubwa.

 Hapa wachezaji wa Azam wakishangilia ushindi dhidi ya Simba, ni baada ya kutoka 2-2 dakika 120 na kuingia katika mikwaju ya penalt ndipo Azam wakaingia fainali kutetea ubingwa wao wa mwaka jana kwa penalt 5-4 uwanja wa Amaan Unguja jana usiku..

Uhuru suleiman na Ibrahim Mwaipopo wakimdhibiti mchezaji wa Simba Ramadhan Singano 'Messi' huku kocha wake 'Julio' akiangalia uwezo wa mwanae pembeni.

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Azam FC wanasubiri mshindi wa leo usiku kati ya Tusker na Miembeni ili wawze kucheza fainali katika kilele cha sherehe za Mapinduzi tarehe 12 jan, 2013.

Picha zote kwa hisani ya Binzubeiry blog.
maelezo kidojembe.

No comments:

Post a Comment