Mtazame vizuuuri huyu jamaa alievaa shati la kijani na kitambaa mkononi. Ni askari, alipigwa kwa bahati mbaya na askari wenzie akidhaniwa ni mwanafunzi. Alipoona kipigo kinazidi akapiga yowe 'jamani eennhhh mtaniua mimi ni askari mwenzenuuu' ndipo alipoachiwa na hapo ameumizwa katika taya anaokotewa vitu vyake vilivyoanguka na kuharibiwa na askari.
Punde na yeye akaanza kuwadunda wanafunzi kwa nguvu bila kutazama kama hao ni binaadam wenzie na wanasikia maumivu. Ameshasahau maumivu aliyoyapata ama sijui ndiyo anamaliza hasira zake kwa wanafunzi... mhh...
Hapa anamuinua mwanafunzi aliezidiwa na moshi wa mabomu ya machozi tena anamuinua kwa maneno makala na matusi utadhana anasikia huyo mwanafunzi, maskini ya Mungu alikuwa amezirai....
Wanafunzi wakitimua vumbi... ahahaaa sicheki kwa furaha, nacheka uchungu. Maisha yangu nilikuwa nikisikia tu mtu anatimua vumbi nilijiuliza sana mtu anatimuaje vumbi, jana ndiyo nilishuhudia.
Huyu dada alikuwa amejificha akachopolewa na kutembezewa kichapo. Nilijiuliza sana mantiki ya kutolewa mafichoni na kupigwa. Maana ninavyofahamu mimi kazi ya jeshi la kutuliza ghasia ama kwa kizungu 'ant riots' kazi yao ni moja tu, kutawanya watu; sasa huyu mpaka amejificha maana yake hapendi vurugu na kwa lugha nyingine alikuwa ametawanyika. Ndipo nikasema kunahitajika elimu kwa askari wa Tanzania juu ya kudhibiti vurugu....
Picha zote kwa hisani ya Said Powa Blog.
No comments:
Post a Comment