Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeondolewa kwenye
fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi
ya nyumbani CHAN.
Stars
imetoka sare ya kutofungana bao lolote na Burundi
katika mechi ya raundi ya pili iliyochezwa katika uwanja wa taifa ya Nyayo
mjini Nairobi .
Timu
hiyo ya Kenya
itajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga lakini wakosoaji wasema Stars
ilikosa kufanya vyema kutokana na maandalizi mabaya.
Kocha
mkuu wa timu ya taifa ya Henri Michel kutoka Ufaransa alijiuzulu na kuondoka
bila kwa heri na hivyo kuiacha timu hiyo bila mkufunzi kwa muda.
Timu
hiyo ya Kenya imekuwa chini
ya uongozi wa kaimu kocha mkuu James Nandwa ambaye aliongoza kikosi hicho
kufika fainali ya kuwania kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA,
mjini Kampala , Uganda .
Kufikia
wakati wa mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzio.
Ratiba ya raundi ya mwisho
Timu
itakayoshinda itafuzu kwa fainali za mashindano hayo ya CHAN yatakayofanyika
Afrika Kusini mwakani.
Mechi
zingine za kanda ya Afrika Mashariki ni mshindi kati ya Eritrea na Ethiopia
atakutana na Rwanda huku Uganda ikipambana na Tanzania kuamua watakaosafiri
Afrika Kusini.
Bingwa
mtetezi wa mashindano ya pili ya CHAN yaliyofanyika mwaka wa 2011 nchini Sudan ni Tunisia
iliyoshinda Angola 3-0 mechi
ya fainali mjini Khartoum .
Mashindano
ya kwanza ya CHAN yalifanyika mwaka wa 2009 na katika mechi ya fainali DR Congo
ilishinda Ghana 2-0 kwenye
mechi ya fainali mjini Abidjan .
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment