Bunge la Venezuela
litaanza kikao huku wasiwasi ukizidi ikiwa Rais Hugo Chavez ataweza kuanza
muhula wake wa pili wa uongozi au la.
Bwana Chavez
anauguzwa Cuba baada ya
kufanyiwa upasuaji kutoa saratani, na inafikiriwa huenda akawa mgonjwa sana na hataweza
kuhudhuria sherehe ya kuapishwa juma lijalo.
Hata
hivo makamo wa rais, Nicolas Maduro, alisema Bwana Chavez anaweza kuapishwa
baadae mbele ya mahakama makuu, na alikataa wito wa upinzani kwamba kufanywe
uchaguzi mwengine.
Mwandishi
wa BBC, Sarah Grainger, akiwa mjini Caracas ,
anasema ufunguzi wa kawaida wa bunge la taifa umekuwa muhimu safari hii kwa
sababu ya Bwana Chavez kukosekana.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment