Shirika la msaada la
kimataifa, Oxfam, linasema kuwa watu 100 tajiri kabisa duniani walipata fedha
za kutosha mwaka jana za kuweza kumaliza ufukara wa watu maskini kabisa
duniani, mara nne zaidi.
Oxfam inasema kuwa
mwaka jana pato la matajiri wakubwa kabisa 100 lilikuwa jumla ya dola 240
bilioni.
Na watu maskini kabisa
wanatumia dola moja na robo tu kwa siku.
Katika taarifa
iliyotoa kabla ya mkutano wa kiuchumi wa Davos, Usiswi, juma lijalo, Oxfam
imesema kuzidi kwa utajiri mkubwa duniani unazuwia juhudi za kupambana na umaskini.
No comments:
Post a Comment