Wabunge nchini Kenya
wamejizawadia dola 107,000 kama marupurupu katika mojawpao ya vikao vyao vya
mwisho vya bunge hilo
kabla ya uchaguzi mkuu kufayika mwezi Machi.
Kila mbunge ataweza kupata mlinzi wa maisha, pasi ya
kidiplomasia na kupata huduma za juu zaidi katika viwanja vye ndege kote
duniani. Haya ndiyo mapendekezo yaliyo katika mswaada waliopiitisha ukisubiri
kuidhinishwa na rais Mwai Kibaki
Ni mara ya pili wabunge wamepitisha mswaada
huu wa kujizawadia mwishoni mwa vikao vyao vyabunge . Rais Mwai Kibaki
alitupilia mbali mswaada wa kwanza kama huu
ambao ulizua ghadhabu miongoni mwa wananchi.
Wabunge
wa Kenya
ni miongoni mwa wabunge wanaopokea mishahara ya juu zaidi barani Afrika kila
mmoja akipata dola elfu kumi na tatu kila mwezi.
Lakini
mshahara wa mkenya wa kawaida ni takriban dola 1,700 kila mwezi.
Mswaada
huu, ulipitishwa siku ya Jumatano na wabunge chini ya thelathini waliokuwa
bungeni. Walikarabati bunge lao kwa kutumia dola milioni kumi na mbili
kulingana na stakabadhi za bunge zilizotolewa hapo jana.
Malipo
haya ni sawa na yale yaliyokuwepo katika mswaada walioupitisha mwezi Oktoba, lakini
wakati huu wabunge hao pia wamependekeza marupurupu kwa rais ambaye atalipwa
dola laki tatu sawa na makamu wa rais na waziri mkuu.
Alipotupilia
mbali mswaada wa kwanza , Rais Kibaki lisema kuwa haiwezekani kwa wabunge
kulipwa mamilioni ya dola wakati uchumi ungali umedumaa.
Tume
ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa umme, iliambia wakenya kuwa hakuna
uhakika ikiwa hatua yao
inakuika katiba.
Mashirika
ya kutetea haki za kibinadamu yameelezea kukerwa sana na hatua ya wabunge. Tayari waziri mkuu
Raila Odinga amepinga mswaada huo akisema kuwa ni kama
uhalifu dhidi ya wakenya na kwamba anashauriana na rais Mwai Kibaki kuhusu
hatua itakayokuwa sawa kwa wakenya.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment