Marais wa Sudan na Sudan
Kusini wameafikiana kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana.
Viongozi hao walimaliza mkutano wao wa siku
mbili mjini Addis Ababa Jumamosi.
Mvutano
baina ya nchi mbili hizo umekuwa tishio kubwa katika eneo lao.
Wapatanishi
wa Umoja wa Afrika (AU) wataweka ratiba ya kutekeleza makubaliano yote ambayo
bado hayakufwatiliwa.
Ratiba
hiyo itakuwa tayari mwisho wa juma lijalo, kwa mujibu wa taarifa ambayo BBC
imeiona.
Ikiwa
ratiba itafuatwa, basi mpaka baina ya nchi mbili hizo rasmi utakuwa eneo la
amani, na Sudan Kusini itaanza tena kuchimba mafuta na kuyasafirisha kwa
kupitia Sudan .
Juba
iliacha kuchimba mafuta mwaka jana kwa sababu ya ugomvi wake na Khartoum kuhusu kiasi gani inafaa kuilipa Sudan kwa kusafirisha mafuta yake kwa kutumia
miundo mbinu ya Sudan .
Miezi
mitatu baadae majeshi ya nchi hizo yakaanza kupigana mpakani na kutia ulimwengu
wasi-wasi.
Mpatanishi
wa AU, Thabo Mbeki, amesema nchi zote mbili zimekubali kuheshimu makubaliano
yaliyotia saini Septemba mwaka jana.
Na
suluhu kuhusu Abyei ni kwamba itawekwa serikali ya pamoja kutawala eneo hilo na maeneo mengine
yenye utata.
Kwa
hivo kwa ufupi marais wote wawili wameafikiana kutekeleza makubaliano
yaliyofikiwa awali.
Chanzo: BBC swahili
No comments:
Post a Comment